HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 04, 2013

POLISI WAMPA KIPIGO MWANDISHI WA CHANNEL TEN AKIWA KAZINI

Mwandishi na mpiga picha wa kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Eliah Ruzika (pichani) amepigwa na askari wa Jeshi la Polisi akiwa kazini kwenye mkutano wa wafanyakazi wa Tazara. Tukio hilo lilitokea Agosti 2.

"Nilipoona vurugu zinaweza kutokea mkutanoni, niliamua kuondoka kumbe askari walikuwa wakinifuatilia kwa nyuma na nilipofika katika Trafic Light za Tazara askari walinivamia na kunikamata na kuanza kunipa kipigo na kunilazimisha niwape mkanda uliorekodiwa kwenye tukio, ndipo nilipogoma na kufanya hivyo na kuanza kunipa kipigo huku wakiwa wamenifunga pingu".

Akizungumza na Habari Mseto Blog Eliah alisema kuwa "nawashukuru wafanyakazi wa Tazara, raia wema na abiria waliokuwa wakisubiri daladala katika eneo la Tazara  kwa kuweza kuniokoa pamoja na  ambao walimpa msaada baada ya kuona mwandishi huyo akipata kipigo licha ya kujitetea kuwa alikuwa katika majukumu yake ya kikazi. "Asanteni sana wananchi mliojitokeza kunisaidia kwani hali yangu ingekuwa mbaya kutokana na kipigo nilichokuwa napata kutoka kwa askari hao ambao walikuwa wamenifunga pingu na kunipa kichapo" alisema Eliah.

"Tunasikitika sana kuona kwamba wote tunaitumikia serikali moja lakini wengine wanatumia vibaya mamlaka waliyonayo. Kwa bahati nzuri mkanda walioutaka hawakuupata na picha za askari waliofanya tukio hilo zipo hatuziweki hadharani kwa makusudi mema. aliongeza Eliah".


Katika tukio hilo Eliah alipoteza alipata maumivu makali katika goti la upande wa kushoto, kupotelewa kwa fedha, baadhi ya vifaa vya kazi kuharibiwa pamoja na kuchaniwa nguo

No comments:

Post a Comment

Pages