Na Bryceson Mathias, Mvomero
MAANDAMANO ya amani ya Wananchi na Wakulima kwenda Kituo cha Polisi Turiani katika Halmashauri ya Manispaa ya Mvomero Morogoro wakipinga wafugaji kulisha eka tatu za mahindi ya Mkulima, Alex Kazimhesa, yalihitimishwa kwa mabomu ya machozi, vipigo na risasi za Moto kutoka jeshi la Polisi.
Mbali na kupinga Ng’ombe wafugaji kula eka tatu za Mahindi ya Kazimheza aliyeachwa Maskini, wanapinga Nguvu ya Dolan a Viongozi wa Mkoa wa Morogoro kuwatetea wafugaji wanaolisha mazao yao wakiwa na Silaha za Moto, kinyu na taratibu na sheria za nchi.
Maandamano hayo yaliyokuwa hayana baraka za jeshi la polisi, isipokuwa harisira za kuharibiwa mazao na Miwa yaliyoanzia vijiji vya Mbogo na Kisala saa 3 asubuhi hadi Polisi Turiani na kufunga barabara za Mvomero Handeni, wakimtaka Mkuu wa Mkoa, Joel Bendera, aende atoe tamko nani ana uhalali eneo hilo wafugaji au wakulima.
Kufuatia hali hiyo, polisi wa FFU waliokuwa na silaha za kivita na mabomu ya kutoa machozi, walilazimika kupambana na maelfu ya wananchi hao, huku raia wakirusha mawe na polisi nao wakirusha mabomu
Dosari ilikuja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bendera kutofika na badala yake alikwenda Mkuu wa Wilaya, Antony Mtaka, na Polisi wa Jeshi Kutuliza Fujo (FFU) ambapo walianza kuwashambulia wananchi kwa Mabomu na kuwapiga na virungu na Risasi za Moto kupigwa juu ili kutuliza fujo na kufungua Barabara magari yapite kuendelea na safari zao.
“Mkuu wa Wilaya ya Mvomero alifanya makosa kuwaruhusu Polisi kuwapiga wananchi bila kusikiliza Malalamiko yetu, hali ambayo imeonesha Serikali inawatetea wafugaji watuharibie mazao wakati hawana uhalali wa kukaa tulipo.
Mahindi yangu yalikuwa tayari yamefikia kuchomwa hata kuanika na kupata Chakula, lakini mwenye pesa siyo rafiki yako, wafugaji juzi wamelisha Ng’ombe eka zangu zote mahindi, nimeachwa Maskini”.alisema Kazimkazi kwa masikitiko.
Hadi tunakwenda mitamboni wananchi walikuwa wmetawanyika na wengine kujificha wakikimbia nyumba zao hapo Turiani, na Polisi walikuwa wakilinda Kituo chao, kusitokee labsha yoyote.
.
Ghasia hizo zilizodumu zaidi ya saa moja, huku polisi hao waliokuwa wakiongozwa na Uongozi wa Polisi Wilaya ya Mvomero (OCD) na Makamanda wake, walifanikiwa kuwadhibiti wafuasi hao kwa kuwatawanya ingawa nguvu kubwa ilitumika huku milio ya risasi na Mabaomu ikisikika katika viunga vya Turiani.
Chadema Yasema;
Kufuatia hali hiyo, viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Sunguaji ukiongozwa na Mwenyekiti wake, Musa Komb, umemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwahamisha Viongozi wote wa Mkoa wa Morogoro na Wilaya zake wakiwemo Makamanda wa Jeshi la Polisi kwa kushindwa kudhibiti Migogoro ya Wafugaji na Wakulima mkoanina wilayani humo. Hivyo wafumuliwe.
Akizungumzia tukui hilo, Kombo alisema, Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Antony, hakuwa na sababu ya kuamuru FFU kuanza kuwapiga na Mabomu na Virungu waandamanji hao, badala yake angewasiliza malalamiko yao, na iwapo hawakuridhiana ndipo angechukua hatua zingine za Ki-Usalama.
Kombo alisema, Mtaka alikuwa anatekeleza Agizo la kuhalalisha kuwa wafugaji wana haki kuwakandamiza na kuharibu mazao yao waathiriwe na Njaa, jambo ambalo Kamanda wa Polisi wa Turiani aliyedai si Msemaji alimtetea Mtaka akidai hakuwa na la kufanya zaidi ya Uamuzi huo.
Wilaya ya Mvomero imekuwa na Mgogoro sugu baina ya Wafugaji na Wakulima, ambapo hata Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Amos Makalla, aliwahi kukiri kwenye mikutano yake na wananchi waSungaji kuwa, Mgogoro huo hata Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amaeshindwa kuutatua.
No comments:
Post a Comment