WASANII wa muziki wa hip hop na bongo fleva nchini, wakutana na kutengeneza wimbo maalumu unaokwenda kwa jina la ‘Tokomeza zero’ kwa lengo la kuhamasisha wanafunzi mashuleni kupenda shule, kuithamini elimu, mwisho wa siku kufaulu mitihani yao.
Baadhi ya wasanii ambao wameimba wimbo huo ni Kala Jeremiah, Stamina, Mwana FA, Roma Mkatoliki, Linex Mjeda, Peter Msechu, Mwasiti, Maunda Zoro, Diamond Platinum, Linna na wengine.
Akuzungumza jijini Dar es Salaam jana, Kala Jeremiah alisema wameamua kufanya hivyo ili kuwahamasisha wanafunzi kusoma kwa bidii na kufanya vizuri katika mitihani yao.
“Unajua ukiwa shule unachezea sana hiyo nafasi lakini ukishafuka mtaani inajua umuhimu wa shule na utatamani kurudi tena umri unakua ushaenda, tunaamini kwa kufanya hivi wanafunzi wanaweza kuhamasika,” alisema Kala Jeremiah.
Alisema kazi hiyo itaanza kusikika na kuonekana mwishoni mwa mwezi huu, wapenzi wa muziki wa bongo fleva na hip hop wakae mkao wa kula kuipokea kazi hiyo ambayo wanaamini kwa asilimia kubwa itachangia wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani yao.
No comments:
Post a Comment