- Sasa kuongozana na Mawaziri mguu kwa mguu
- Asema kazi yake ya kuijenga chama inahitaji watu makini kama mtu hawezi kasi yake awapishe.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikaribishwa kwa kahawa katika kijiji cha Budalabujiga wilaya ya Itilima mkoani Simiyu ambapo Katibu Mkuu alifanya ziara ya siku moja wilayani hapo.Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikaribishwa kwa kahawa katika kijiji cha Budalabujiga wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, Katibu wa Itikadi na Uenezi ameongozana na Katibu Mkuu wa CCM katika ziara ya mkoa wa Simiyu.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo wakati akikagua Bwalo la chakula la shule ya sekondari ya kata ya Kanadi, wilayani Itilima mkoa wa Simiyu. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya kata ya Kanadi baada ya kutembelea bwalo na bweni la shule hiyo ambapo aliwasihi wanafunzi kusoma kwa bidii na kuahidi kuwapatia sola.Katibu Mkuu wa CCM akiwa amembeba mtoto Dhahabu katika kituo cha afya cha Nangale wilaya ya Itimila mkoani Simiyu.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye mavazi yake ya uchifu baada ya kusimikwa Uchifu na kutambulika kama Chifu Machibola katika kijiji cha Migato wilaya ya Itilima mkoa wa Simiyu, Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya mkoa wa Simiyu ambapo moja ya lengo la ziara yake ni kukagua na kuimarisha uhai wa chama na kusimamia ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2010. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akinywa maji kwa kutumia kipeyu katika kijiji cha Migato wilaya ya Itilima mkoa wa Simiyu.Katibu Mkuu ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupiga lipu kwenye ujenzi wa ofisi za Halmashauri za wilaya ya Itilima mkoani Simiyu.
September 18, 2013
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment