MKURUGENZI wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Sunday Kayuni
DAR ES SALAAM, Tanzania
Madhumuni ya warsha hiyo ni kuainisha majukumu yao , kubadilishana uzoefu, ikiwamo pia kuwapa ‘methodolojia’ mpya ya ufundishaji na muongozo kuhusu mfumo wa leseni za makocha ambao watautumia katika nchi zao
MKURUGENZI wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
Sunday Kayuni ameteuliwa kushiriki Warsha ya Wakufunzi wa Makocha wa Shirikisho
la Soka Afrika (CAF), itakayofanyika kuanzia Oktoba 22 hadi 24 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam leo, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, alisema kuwa warsha hiyo
iliyoandaliwa na CAF kwa ajili ya wakufunzi wake itafanyika nchini Cameroon,
ikishirikisha wakufunzi 18 wa CAF.
Wambura alibainisha kuwa, madhumuni ya warsha hiyo ni
kuainisha majukumu yao ,
kubadilishana uzoefu, ikiwamo pia kuwapa ‘methodolojia’ mpya ya ufundishaji na
muongozo kuhusu mfumo wa leseni za makocha ambao watautumia katika nchi zao.
Mbali ya Kayuni wa Tanzania, wakufunzi wengine kwa mujibu wa
taarifa ya CAF kwa TFF ni Ahmed Babiker (Sudan), Amadou Shaibu (Nigeria), Boy
Bizzah Mkhonta (Swaziland), Duodu Fred Osam (Ghana), Edussei Anthony (Ghana) na
Fathi Nossir (Misri).
Wengine ni Faouzy Altaisha (Sudan), Fran Hilton Smith
(Afrika Kusini), Francis Oti-Akenteng (Ghana), Honour Janza (Zambia), Kasimawo
Laloko (Nigeria), Mahmoud Saad (Misri), Paul Hamilton (Nigeria), Serame
Letsoaka (Afrika Kusini), Shawky Abdel Shafy (Misri), Thondoo Govinder
(Mauritius) na Ulric Mathiot (Shelisheli).
No comments:
Post a Comment