Makamu Mwenyekiti wa kundi la wabunge wa Tanzania
wanaojihusisha na hifadhi endelevu ya maliasili na matumizi endelevu ya
mazingira (TPGSNRC), Othman Mfutakamba akiangalia meno ya tembo wakati wa
maadhimisho ya siku ya tembo kitaifa iliyokuwa na kaulimbiu ‘Jiunge katika
mapambano dhidi ya ujangili wa tembo’ yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Mlimani
City jijini Dar es Salaam. Katikati
ni Meneja wa Bia ya Ndovu, Pamela Kikuli ambao walidhamini maadhimisho hayo. Kulia ni askari wa Wanyamapori, Emmanuel
Katambi. (Picha na Francis Dande)
Gari la Maliasili likiwa limebeba Meno ya Tembo, wakati wa kujiandaa na Maandamano kuelekea Mlimani city kwa ajili ya maadhimisho hayo
Msanii wa Muziki wa Kitanzania Mrisho Mpoto akianza kuongoza maandamano kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam Kuelekea Ukumbi wa Mlimani City leo.
Maandamano
Maandamano ya Siku ya Tembo yakiwa yanaendelea kuelekea ukumbi wa Mlimani City kwa ajili ya Kongamano hilo
Wasanii wa Mrisho Mpoto wakiwa wamebeba chatu katika maadhimisho ya Siku ya Tembo Kitaifa leo
Mkurugenzi wa wanyamapori Wizara ya maliasili na utalii Prof. Alexander Songorwa akisoma Hotuba kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na utalii.
Wadau mbalimbali wa utalii na kupinga mauaji dhidi ya Tembo wakiwa wanafuatilia kwa umakini maadhimisho ya Siku ya Tembo kitaifa.
Wanafunzi kutoka Shule ya Jitegemee wakiwa wanafuatilia kwa umakini Maadhimisho hayo.
Picha ya Pamoja ya Viongozi Mbalimbali wa Serikali na wadau
No comments:
Post a Comment