Karama Nyilawila akiruka juu baada ya kutangazwa mshindi wa ubingwa wa dunia wbfed middle weight katika pambano lililofanyika ulaya.
Aliyekuwa bingwa wa Dunia, middle weight bondia Karama Nyilawila amesema ana hamu kubwa ya kumdunda mtoto wa manzese Thomas Mashali (ambaye ni bingwa wa Afrika wbfed middle weight) aliyeutwaa hivi karibuni kwa kumshinda Mada Maugo ,
Mashali akizungumza na vyombo vya habari ameeleza kuwa mashali ameupata ubingwa huo kibahati na haukubali uwezo wake na alishawahi kucheza na mashali alikuwa hayupo fiti alipigana akiwa na malaria na akatoka nae sare katika maamuzi ya utata kwa kuwa alikuwa kwao,
Karama nyilawila ambae hivi karibuni atakuwa na pambano dhidi ya Sado philemon tarehe 20 ya mwezi huu wa kumi katika ukumbi wa ccm mwinjuma,pambano liloandaliwa na Ibrahim kamwe wa bigright promotion aliendelea kusema pambano hili akifanikiwa kumpiga sado hataupoteza ufiti wake kwa ajili ya mapambano yatakayofuata likiwemo la hasimu wake Thomas mashali.



No comments:
Post a Comment