HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

June 21, 2026

CRDB Yawakatia Bima na Kuwapa Mtaji Mapacha Watano wa Simon Mkwizu

Familia ya Simon Mkwizu, mwendesha bodaboda kutoka Dar es Salaam aliyepata watoto mapacha watano katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, imepata sababu ya kutabasamu baada ya Benki ya CRDB kuipatia msaada mkubwa wa kifedha na kijamii.



Katika hafla maalumu iliyofanyika Muhimbili, Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile, alitangaza kuwa watoto wote watano pamoja na mama yao watapatiwa bima ya afya kwa kipindi cha miaka mitatu.



Mbali na hilo, kila mtoto atafunguliwa akaunti ya Junior Jumbo yenye amana ya Sh milioni 1.5, huku mama yao Victoria akifunguliwa Akaunti ya Malkia yenye Sh milioni 2.5 na akaunti nyingine ya ujasiriamali yenye Sh milioni 1.5.



Kama sehemu ya kumuinua kiuchumi baba wa familia, CRDB pia imemkabidhi Simon Mkwizu bajaji mpya itakayomsaidia kuongeza kipato na kuhudumia familia yake.


Akizungumza kwa furaha, Mkwizu alisema msaada huo umefika wakati muhimu na kuipa familia yake matumaini makubwa ya maisha bora. Pia aliishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa huduma bora ambazo zimeendelea kutolewa kwa mke wake na watoto tangu walipozaliwa.



Hospitali ya Muhimbili imesema itaendelea kugharamia matibabu ya mama na watoto hao hadi watakaporuhusiwa na kuwataka wadau wengine kuendelea kujitokeza kusaidia familia hiyo.



No comments:

Post a Comment

Pages