MADIWANI wa Mvomero wamemtwisha Zigo Rais, Jakaya Kikwete, wakimtaka amalize Mgogoro wa Wakulima na Wafugaji, ili wapumzike kupopolewa Mawe na Mishale ya Makundi hayo kila kuchwapo.
Wamedai wenye maamuzi huipa kisogo migogoro inapoibuka na hivyo na kuwaachia wao wasio na maamuzi wakabiliane nayo, huku wao wakionja Joto ya Jiwe wanapokabiliana nayo wakiwa pekee yao.
Bila kumtaja Naibu Waziri wa Habari Michezo, Utamaduni na Vijana na Mbunge wao, Amosi Makalla na viongozi wengine, Madiwani hao wakihojiwa jana kwa sharti la kutotajwa walisema, Migogoro hiyo ikitokea, Viongozi wao jimboni, wilayani na mkoani, huwa wako nje.
“Diwani Athumani Mkimbu, Kata ya Sungaji alijeruhiwa kwa Mishale na Mapanga kichwani na kushonwa nyuzi 12, Diwani wa Mtibwa, Luka Mwakambaya, alikurupushana nao, na juzi Diwani, Juma Malaja, Kata ya Hembeti alipopolewa Mawe na kushonywa nyuzi Nne mbali ya Makofi aliyopigwa”.alisema
“Ingawa wazazi ni Baba na Mama, inapofika kwetu madiwani adha hizi zikitokea Wakubwa wetu wenye maamuzi huwa wako Dar es Salaam, Safarini, Iringa au kwenye Michezo, hivyo sisi ndio tunaobaki kujeruhiwa na Mapanga, Mikuki na Mawe huku wenzetu wakiwa salama”.
Alisema, ni kweli waliomba kuwa Viongozi kwa nia jjema ya kuwatumikia wananchi na kuwapa madaraka viongozi wao, lakini alidai hadi wanaondoka madarakani watakuwa wamepata Pensheni ya Ulemavu, huku wakikosa hata mkono wa kwaheri kama wakulima wenyewe.
Mmoja alisema, anaandaa Hoja Maalum ili watakapokutana kwenye kikao cha Baraza la Madiwani 18.10.2013, Serikali kupitia kwa Mkurugenzi, iwahakikishie Usalama wao na hatua dhidi ya Wakulima na Wafugaji wanaowajeruhi, tofauti na kesi za kuwaumiza kusuasua.
Aidha karibuni Wakulima hao Walilipopoa Mawe hata Gari la Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Antony Mtaka na Mkurugenzi wake, Wales Karia, huku Diwani wa Hembeti Malaja na Mwenyekiti wa Kijiji cha Dihombo, Pantareo Mathias wakipopolewa Mawe na Makofi, huku wananchi wakidai tatizo ni viongozi wao kukosa maamuzi magumu.
No comments:
Post a Comment