HABARI MSETO (HEADER)


October 15, 2013

MAONESHO YA TANZANIA HOMES EXPO YAFUNGULIWA RASMI

Maonyesho makubwa ya sekta ya nyumba yajulikanayo kama Tanzania Homes Expo yamefunguliwa rasmi na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa 

Akiongea baada ya kutembelea mabanda mbali mbali alisema ‘’ Inafurahisha kuona watoa huduma mbalimbali binafsi na wa serikali wako hapa kutoa taarifa na kuonyesha masuluhisho mbali mbali ya ujenzi. Napenda kuchagiza umuhimu wa kutumia Tehama katika kuboresha maisha ya wakazi’’.

Mkurugenzi Mtendaji wa EAG Group ambao ni waandaaji na wamiliki wa Tanzania Homes Expo alisema ‘Ukuaji wa idadi ya watu na upatikanaji wa makazi havina uwiano sawa, hii ni changamoto ambayo inaweza kutatuliwa kwa kuwawezesha wananchi kuwa na makazi  hivyo maonyesho ya Tanzania Homes Expo yanawawezesha wananchi kukutana na kufahamu huduma au kupata ushauri wa sekta pana ya makazi’.


Maonyesho ya Tanzania Homes yamedhaminiwa na CAM Gas, Camel Cement, African Life, CRDB na NHIF.Maonyesho hayo yameanza tarehe 14 na yataisha tarehe 15
 Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano Prof. Mbarawa akifungua maonyesho ya Tanzania Homes Expo. Kushoto ni Imani Kajula Mkurugenzi Mtendaji wa EAG Group, Kulia ni Oscar Mgaya Afisa Mtendaji Mkuu wa TMRC. Wengine ni viongozi wa Camel Cement and CAM Gas.
 Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Universal Electronics & Hardware, Mercy Muro akifafanua jambo kwa watu waliotembelea banda lao.
 Baadhi ya wateja wakiwa katika banda la Mbezi Tiles.
 Maofisa wa Kampuni ya Universal Electronics & Hardware wakiwa pamoja.
 Meneja Msaidizi benki ya Exim, Hosiana Muro akifafanua (kushoto), jambo kwa watu waliofika katika Maonesho ya Sekta ya Nyumba, jijini Dar es Salaam, kuhusu mikopo ya nyumba wanayoitoa.
Wadau wa maonesho ya Sekta ya nyumba, Multchoice Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Pages