Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Yusuf Bakhresa akisalimiana na wasanii wakati wa ufunguzi wa Ofisi ya AZAM TV.Baadhi ya wasanii maarufu nchini wakiwa na Meneja wa Uhusiano wa AzamTV, Maryam El-haj wakati wa ufunguzi wa Ofisi ya AZAM TV.
DAR ES SALAAM, Tanzania
WASANII wa filamu nchini, wamekiri kufurahishwa kwao na ujio wa kituo cha Teevisheni cha Azam (Azam Tv) na kuutaja kama ukombozi utakaochagiza maendeleo ya sanaa na wasanii ndani na nje ya nchi.
Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa Makao Makuu ya Kampuni ya
Azam Media Ltd, wasanii hao, Jacob Steven ‘JB’, Mahsen Awadh ‘Dk Cheni’, Yvone
Cherry ‘Monalisa’ na Suzan Lewis ‘Natasha,’ walisema kama wasanii wanatarajia
mengi yaliyo bora kutoka Azam Tv.
Kwa upande wake JB alisema sanaa ya Tanzania hususani ya
filamu na wadau wake, wamepata sehemu muhimu itakayosaidia kukuza sio tu
kiwango cha ubora wa kazi zao, bali pia pato la wasanii kutokana kutokana na
mikataba ya matangazo ya muvi zao.
“Tuna matumaini makubwa kwamba ujio wa Azam Tv ni moja ya
njia zitakazoboresha kazi na pato la wasanii. Ni fursa nyingine ambayo wasanii
tunapaswa kuitumia vema ili kuwafikia wadau wetu kupitia,” alisema JB mmoja wa
wasanii nguli wa Bongo Muvi.
Monalisa, yeye alibanisha kuwa matarajio ya wasanii wengi ni
kuwa ujio huo wa Azam Tv utakwenda sambamba la ongezeko la mikataba ya kurushwa
kwa filamu zao, kwani kabla ya hapo kulikuwa na mikataba michache.
“Naamini hii ni moja ya neema miongoni mwa wasanii, lakini
kwa sanaa na wadau wake kwa ujumla. Tutapata mikataba minono ya kurushwa kwa filamu
zetu hapa na kutanua pato letu. Hakika nimefurahia ujio wa Azam Tv,” alisema
Monalisa.
Dk Cheni naye hakuwa mbali na maoni ya wenzake, akisema
anaamini fursa ya wasanii kuwafikia wadau na wadau kupata vilivyo bora kutoka
kwao imepata kiunganishi muhimu ambacho ni Azam Tv.
“Kwangu mimi Azam Tv ni zaidi ya kituo cha Televisheni.
Nakichukulia hiki kama kiunganishi muhimu cha sisi kuwafikia mashabiki wetu,
lakini wao pia kutuona kwa mapana na kuchangia maendeleo ya sanaa na wasanii
Tanzania,” alisema Dk Cheni.
Natasha yeye kwa upande wake aliupongeza uongozi wa Azam
Media kwa kuwajali wasanii kwa kuanzisha chaneli ya Sinema Zetu inayopatikana
katika king’amuzi cha Azam Tv na kwamba anaamini itakuwa chachu kuu ya
mafanikio ya sanaa nchini.
No comments:
Post a Comment