HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 28, 2013

MAMA WA MITINDO ASIA IDAROUS KHAMSINI:>KUPAMBA USIKU WA REAL UNIQUE TANZANIA, REGENCY HOTEL LEO
 *SKYLIGHT BAND KUTOA BURUDANI

Na Andrew Chale

MBUNIFU mkongwe wa mitindo na mavazi nchini, Asia Idarous Khamsin, usiku wa leo  Desemba 28 anatarajiwa kupamba  shoo kali kwa kuonesha mavazi  kwenye Usiku wa Real Unique Tanzania’  utakaofanyika ndani ya  Regency  Hotel, jijini  Dar es Salaam huku ukisindikizwa na  Skylight Bend.

Akielezea juu ya onesho hilo la ‘Usiku wa Real Unique Tanzania’ , Asia ‘Mama wa Mitindo’ alisema kuwa itakuwa ni ya kipekee katika kufunga mwaka wa 2013 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2014.

“Ni hatua ya kipekee kwa mimi kuweza kuonesha shoo yangu hii leo katika “Usiku wa Real Unique Tanzania” kwani ndio shoo ya funga mwaka, hivyo wadau wa mitiondo na mavazi watapata kufurahia onesho hilo sambamba na burudani kali kutoka kwa bendi maalufu ya Skylight.” Alisema Asia Idarous.

Mbali na kupamba shoo hiyo kwa kuonesha mavazi yake, Asia Idarous pia ndiye mgeni rasmi kwenye usiku huo wa funga mwaka wa Real Unique Tanzania.

Aidha, katika shoo hiyo, kiingilio  ni shilingi 25,000. Huku kwa viti maalum,  VIP kikiwa sh  50,000.
 Asia Idarous akiwa na Binti yake.
Asia Idarous akitangaza rasmi wakati wa uzinduzi wa kampuni ya Real Unique Tanzania hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Pages