Simba SC yaja na tamaduni za timu kubwa duniani
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Klabu
ya Simba kwa kushirikiana na Wadhamini wake, MeTL imezindua moja ya
tamaduni zinazofanywa na Klabu nyingine duniani katika kusherehesha
mashabiki wake, kuwapa hamasa na kuleta umoja katika Soka hususani
kuanzia msimu ujao wa mashindano wakianza na Simba Day, 19 Septemba
2021.
Simba
SC imezindua Karagosi (Mascot) waliopewa jina la MO Rafiki, ambao
watatumika kusherehesha Mashabiki wake pindi timu hiyo inapokuwa
Uwanjani katika michezo yake mbalimbali sambamba na kampeni zake za
kutoa misaada kwa makundi maalum.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Barbara
Gonzalez amesema ujio na ubunifu wa ‘Mascot’ hao lengo kubwa kugusa
maisha ya watu, kuleta furaha kila sehemu timu inapokuwa ikicheza na
hata kwenye kampeni zake mbalimbali.
Barbara
amesema, “Tunaona timu zilizoendelea ulimwenguni, timu za Arsenal,
Manchester United, Everton na nyingine, zinafanya ubunifu kama huu ili
kuleta hamasa, umoja kwa mashabiki na hata kwa Wachezaji wanakuwa na
furaha wakiwaona ‘Mascot’ hao.
“Nakumbuka
Mesut Özil alijitolea kumlipa Mascot wa timu ya Arsenal baada ya
kutangazwa hali ya ukata kipindi cha Corona. Tunaona umuhimu wa Mascot
hadi Wachezaji walitaka aimsiondoke ndani ya Klabu”, ameeleza Barbara.
Simba
SC inajiandaa na tamasha lake la Simba Day, Septemba 19, 2021 ambapo
itacheza mchezo wa kirafiki na Kabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo. Tamasha hilo litaenda sambamba na utambulisho wa
Kikosi chake cha msimu wa 2021-2022.
No comments:
Post a Comment