HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 11, 2022

WAZIRI MKENDA AIPONGEZA SHULE YA DIS

Serikali imezipongeza shule binafsi kwa kusaidia kupunguza msukumo wa watu kupeleka  wanafunzi nchi jirani kwenda kusoma.

 

Akizungumza wakati wa mahafali ya Kidato cha Nne na Sita katika Shule ya Dar es Salaam Independent School, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema kuwa shule binafsi zimesaidia sana kupunguza ule msukumo wa watu kupeleka wanafunzi Kenya,Uganda kwenda kusoma.

 

 "Wanafunzi waliomaliza Kidato cha Sita katika Shule ya Dar es Salaam Independent School karibia wote wameshapata usajili katika vyuo vikuu mbalimbali duniani". 

 

Katika mahafali hayo jumla ya wahitimu 90 walikabidhiwa vyeti katika mahafali hayo huku wahitimu 50 wakiwa wanafunzi wa kidato cha Nne na 40 wakiwa kidato cha Sita. 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, akitoa hotuba yake wakati wa mahafali ya Kidato cha Nne na Sita katika Shule ya Dar es Salaam Indepedent School jijini Dar es Salaam leo Juni 11, 2022.

Mkuu wa Shule ya Dar es Salaam Independent School, Catherine Shindika, akitoa hotuba yake wakati wa Mahafali ya Kidato cha Sita na Nne.


Rais wa Wanafunzi Shule ya DIS, Erica Nyaki, akizungumza wakati wa mahafali hayo.

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, akimakabidhi cheti Rais wa Wanafunzi Shule ya Dar es Salaam Independent School, Erica Nyaki, wakati wa mahafali ya kidato cha Sita yaliyokwenda sambamba na yale ya kidato cha Nne.

 

Erica Nyaki, akipokea cheti kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, huku wazazi wake wakishuhudia.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Adolf Mkenda, akimkabidhi cheti mwanafunzi wa Kidato cha Nne Edward Mdoe wakati wa mahafali ya Shule ya Dar es Salaam Independent School yaliyofanyika Mbweni jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wahitimu wa Kidati cha Sita.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Adolf Mkenda, akimtunza mwanafunzi wa kidato cha Nne, Abigael Ndimubenya, baada ya kuvutiwa na uimbaji wake katika mahafali ya kidato cha Sita na Nne ya Shule ya Dar es Salaam Independent School jijini Dar es Salaam. 

Mwanafunzi wa kidato cha Nne, Abigael Ndimubenya, akiwa na cheti  cha mwanafunzi bora katika shughuli za kijamii.

No comments:

Post a Comment

Pages