HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 18, 2013

Mfalme Siboka awakuna mashabiki Mbeya
 Askari akijaribu kuwatuliza baadhi ya mashabiki waliokuwa na munkari wa kutaka kuingia katika onesho la mwanamuziki wa nyimbo za asili, Costa Siboka maarufu kwa jina Mfelme siboka lililofanyika katika ukumbi wa City Pub jijini Mbeya mwishoni mwa wiki. (Picha na Kenneth Ngelesi)
 Mfalme Siboka akiwa na kundi la wanenguaji wakati wa onesho la kuutambulisha wimbo wa asii ya Kinyakyusa unaokwenda kwa jina Twilsile Kukaja.

Na Kenneth Ngelesi, Mbeya


MSANII wa nyimbo za asili nchinbi Tanzania Costa Siboka maarufu kwa jina Mfalme  Siboka  mwishoni mwa wiki alifanya onyesho la kufa mtu na kuweza kuwa pagawisha wakazi wa jiji la Mbeya baada ya kuimba wimbo moja wapo wa Kinyakyusa moja ya makabila makubwa mkoani hapa.

Mbali na kuimbia nyimbo hizo za asili msanii huyo alifanyiwa  mapokezo ya nguvu katika onyesho hilo ambalo lililofanyika katika ukumbi wa City Pub eneo la Mwanjelwa jiji hapa na kuudhuriwa na mamia ya mashabiki.

Mfaume Sibo alianza kupanda jukwaani majira ya saa 3;30 na kupkewa na shangwa na vifijo baada ya kutambulish wimbo wa asili ya kinyakyusa uitwao Twisile kukaja ukiwa na tafsiri ya tumekuja nyumban ambayo ni mpya na ilikuwa nifursa kuitumbulisha kwa wakazi wa Mbeya 

Mbali na yimbo hizo Siboka aliimba nyimbo za asili ya Kisukuma kiking, Kisafywa huku akisindikzwa na wanenguaji kutoka kundi lake hilo ambao wakokena kukonga nyoyo z\a mashabiki wa muziki wa yumbo za asili kutokana na kuvaa kanga moja wakati wa onyesho hilo.


Akizungumza baada  onyesho hilo hilo Siboka alisema kuwa lengo la kuwaburudisha wapenzi wa nyimbo za asili kutoka makabila yote nchini.


Aliongeza kuwa mara baada kumaliziuka kwa onyesho kanda ya Nyanda za Juu kusini, sikukuu ya Christman atakuwea katika visiwa vya ukerewe kwa ajili ya onyesho lingine katika ukumbi wa Afro Beach.

Hata hivyo Siboka alitumia fursa hiyo kuwatamabulisha wadhamini wa onyesho kuwa ni Konyaji ambao ni wadhamini wakuu, CXC Afrika, Afropoa, na Michuzi Blogs.

No comments:

Post a Comment

Pages