HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 18, 2013

NMB YATOA MADAWATI SHULE YA MSINGI MAKUBURI JESHINI
Hivi karibuni, Benki ya NMB imeukabidhi  Uongozi wa shule ya msingi Makuburi Jeshini jijini Dar es Salaam msaada wa madawati yenye thamani ya shilingi million tano. Madawati ambayo yatasaidia kupunguza upungufu wa madawati katika shule hiyo.
 Menejawa NMB Mlimani City Bw. Leonard Ngaya (kushoto) akikabidhisehemuyamadawati 55 yenye thamani ya shilingi milioni tano kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Makuburi Jeshini Bi. Stella Kaluse (kulia). Wakishuhudia makabidhiano hayo ni Mwenyekiti wa Kata ya Makuburi Bw. Moshi Kaftanyi (katikati) naMenejawa NMB tawi la University Bw.  Charles Mapunda .Hafla ya Makabidhiano haya yalifanyikahivi karibuni katika viwanja vya shule hiyo.
Wawakilishi toka NMB pamoja na uongozi wa shule wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi baada ya kukabidhi madawati yaliyotolewa na benki ya NMB kwa ajili ya kupunguza uhaba wa madawati katika shule hiyo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika katika viwanja vya shule ya makuburi Jeshini hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Pages