HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 19, 2013

RAJA CASABLANCA YATINGA FAINALI KLABU BINGWA YA DUNIA, WACHEZAJI WAMVUA VIATU, JEZI RONALDINHO
Mwanasoka Bora wa Dunia wa Fifa wa zamani, Ronaldonho Gaucho anayekipiga na Atletico Mineiro ya Brazil (katikati), akifurahia kuona wachezaji wa Raja Casablanca ya Morocco wakimvua viatu vyake baada ya kumvua jezi aliyovaa wakati wa mechi yao ya Nusu Fainali Klabu Bingwa ya Dunia, ambayo Raja ilishinda kwa mabao 3-1 na kutinga fainali ambako Jumamosi itacheza na Bayern Munich ya Ujerumani.
Mmoja wa wachezaji wa Raja Casablanca ya Morocco, akifurahia kupata kiatu cha mguu wa kulia cha Ronaldonho baada ya kumvua mwishoni mwa mechi yao ya nusu fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia.
Wachezaji wawili wa Raja Casablanca wakifurahia baada ya kufanikiwa kupata kiatu kimoja kila mmoja alivyokuwa amevaa gaucho. Mchezaji wa kwanza kushoto alikuwa na furaha zaidi baada ya kupata na jezi namba 10 ya Atletico iliyokuwa imevaliwa pia na Ronaldinho. 
Wachezaji wa Raja Casablanca wakishangilia kutinga fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia kwa kuwang'oa Mabingwa wa Amerika Kusini, Atletico Mineiro ya Brazil.
Wachezaji na maofisa wa Raja Casablanca, wakishangilia ushindi wao huo dhidi ya Atletico Mineiro ya Brazil na kutinga fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia.
Ronaldinho akiwa haamini macho yake baada ya filimbi ya mwisho ya mechi ya nusu fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia, ambako klabu yake ya Atletico Mineiro ilichapwa mabao 3-1 ambalo alilifunga yeye kwa mkwaju wa adhabu ndogo.
Ronaldinho Gaucho wa Atletico Mineiro, akishangilia bao lake la kusawazisha kwa mkwaju wa 'free kick', ambalo hata hivyo halikutosha kuwapeleka fainali ya klabu bingwa ya Dunia, baada ya Raja kupiga mabao mawili ndani ya dakika tano za mwisho za mechi yao ya nusu fainali. (Picha Zote kwa Hisani ya gazeti la Daily Mail la Uingereza)

RABBAT, Morocco

Wakati Barca ikiwania kuweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza ya Bundesliga kutwaa taji la Klabu Bingwa ya Dunia kesho, wenyeji Raja wanataka kutwaa ubingwa huo ili kuwa klabu ya kwanza Morocco na bara la Afrika kutwaa taji hilo

WENYEJI wa michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia, Raja Casablanca ya hapa, jana usiku walifanikiwa kuzitumia vema dakika 10 za mwisho za pambano lao dhidi ya Atletico Mineiro ya Brazil, na kufuzu fainali ya michuano hiyo itakoumana na Bayern Munich.

Raja, ambayo inashiriki michuano hiyo kwa tiketi ya klabu bingwa ya nchi mwenyeji wa mashindano, walionesha kuwa na uwezo wa kusonga mbele baada ya kuwabana Wabrazil na kumaliza nao dakika 45 kwa sare ya 0-0.

Baada ya mapumziko ikiwa na kujimini kwingi, Raja iliwachukua dakika sita tu kufunga bao la uongozi lililowekwa kimiani na Mouhcine Iajour na kuamsha shangwe za mashabiki wa nyumbani katika dakika ya 51.

Lakini, nyota wa zamani wa Barcelona na AC Milan, ambaye pia ni mshindi wa Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Fifa, Ronaldinho aliisawazishia Mineiro kwa mkwaju wa adhabu ndogo ‘free-kick’ kunako dakika ya 63 na kuwapa matumaini mabingwa hao wa Amerika Kusini.

Raja ikajipatia bao la uongozi wa pili kunako dakika ya 83, wakati nyota wa Mineiro, Rever alipoonekana kumchezea madhambi Iajour, ingawa marudio ya picha za video hayakuonesha mgusano baina ya nyota hao.

Mohsine Moutouali, akafunga kwa penati hiyo kwa ustadi, kabla ya Vianney Mabide kufunga bao la tatu kwa guu la kushoto na kuipeleka Raja fainali inakotarajia kuwavaa mabingwa wa Ulaya Bayern waliotangulia mapema juzi.

Mwishoni mwa mpambano huo, wachezaji wa Raja Casablanca walimzunguka Ronaldinho wakimuomba jezi, kisha kumvua viatu alivyokuwa amevaa na kuugawana kila mmoja akichukua kimoja.

Kwa ushindi huo, Raja kesho Jumamosi inashuka dimbani jijini Marrakesh kuwaa Bayern Munich katika fainali kali inayowapa mashaka Bayern kama wataweza kutimiza nia ya kuwa klabu ya kwanza ya Ujerumani kutwaa ubingwa michuano hiyo.

Hii itakuwa mara ya pili tu ya michuano hii tangu ilipoanza kutumika katika mfumo wa sasa mwaka 2005, kwa fainali kukutanisha timu kutoka mabara yasiyokuwa ya Ulaya na Amerika Kusini kama ilivyozoeleka.

Wakati Barca ikiwania kuweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza ya Bundesliga kutwaa taji la Klabu Bingwa ya Dunia, wenyeji Raja wanataka kutwaa ubingwa huo ili kuwa klabu ya kwanza Morocco na bara la Afrika kutwaa taji hilo.

BBC Sport

No comments:

Post a Comment

Pages