HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 19, 2013

Azam Tv kuanzia ‘Mapinduzi Cup 2013’
Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Yusuph Bakhresa akibadilishana mawazo na wasanii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Yusuph Bakhresa akizungumza na waandishi wa habari.
Salamu kwa wasanii.
Tunazindua.

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Azam Media Ltd, imezindua Ofisi za Makao Makuu na kituo cha televisheni cha Azam, ambacho kitaanza rasmi kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mechi za soka katika michuano ya Kombe la Mapinduzi 2013 visiwazi Zanzibar.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Yusuph Bakhresa, alisema kuwa ujio wa ofisi hizo unatoa fursa ya wateja wao kupata uhakika wa mahali pa kuhudumiwa, huku akiwataka kuipokea Azam Tv iliyosheheni kila kitu.

Alisema wadau wa soka Tanzania wataanza kushuhudia uhondo wa matangazazo ya ‘live’ kuanzia katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, inayotarajia kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa mwaka hadi Januari 12 ambayo nilele cha Sikukuu ya Mapinduzi.

Bakhresa alisema kuwa, ubora wa huduma kupitia Chaneli 52 zinazopatikana katika king’amuzi cha Azam unawapa uhakika wa kutamba katika tasnia ya habari, kupitia vipindi bora na bei nafuu za malipo ya kila mwezi, ambavyo anaamini vitavutia wadau.

Alibainisha kuwa, kupitia chaneli mbili za Azam One na Two, wapenzi wa soka nchini wataona ‘live’ matangazo ya Kombe la Mapinduzi kutoka kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba, ambao pia utakuwa ukishuhudia pia mechi za kwanza kutanmgazwa ‘live.’

Michuano ya Mapinduzi 2013 itashirikisha klabu za Tanzania Bara za Yanga, Azam FC, Mbeya City na Simba, ambazo zitachuana na zile za Pemba Kombaini, Unguja Kombaini, KMKM na nyingine ambayo haijatambulishwa, pamoja na Tusker ya Kenya.

Bakhresa alibainisha kuwa, baada ya kumalizika kwa Kombe la Mapinduzi, Azam Tv itahamia katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom, kote huko wakitarajia kufanya vema kupitia mitambo bora na ya kisasa kuhimili ushindani sokoni.

Aliongeza kuwa, Azam Media itambua ugumu wa tasnia ya habari na ushindani uliopo, lakini wamejipanga na kwamba wana uhakika mitambo yao bora ya kurushia matangazo itawewezesha kukabiliana na yote na hatimaye kuzishinda kampuni kongwe nchini.

No comments:

Post a Comment

Pages