MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Moses
Bushamaga ‘Mez B’ usiku wa kuamkia Jumamaosi alinusurika kuuwawa baada ya
kuvamiwa na watu wasiojulikana, maeneo ya Sinza Vatcan jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam jana baada ya kutoka hospitali, Mez B alisema alivamiwa na watu asiowafahamu
akiwepo baunsa ambaye alimuelekeza cha kufanya mtu huyo ambaye alimjeruhi
vibaya maeneo ya usoni.
“Nilitoka kwa Noorah nilipofika maeneo ya White
Inn, Sinza nikashuka kwenye gari baada ya hapo nikamuona baunsa anakuja mbele
yangu alikuwa na jamaa mmoja hivi, huyo baunsa akamwambi yule jamaa fanya kazi
yako, huyo jamaa akatoa kisu na kuanza kunijeruhi maeneo ya usoni yani hapa
sitamaniki kabisa lakini nashukuru mungu bado napumua,” alisema Mez B.
Alisema wakati yeye anafanyiwa unyama huo,
walinzi wa hapo walimuangalia tu hawakutoa msaada wa aina yoyote mpaka yule
jamaa alipoacha mwenyewe kumfanyia unyama huo.
Mez B ni kati ya wasanii ambao wanatikisa katika
muziki wa bongo flava, kutoka kundi la Chember Squared ambalo lilikuwa
likiongozwa na mkali wa free style, marehemu Albert Mangweha ‘Ngwea’ ma msanii
Athuman Kapongo ‘Dark Master’.
Msanii huyo alishawahi kutamba na ngoma zake
kama ‘Kikukuu cha Mama Rhoda’, ‘Kidela’ na ‘Kama Vipi’ ambao alishirikiana na
mwanadada Rehema Chalamila ‘Ray C’ kabla hajapotea katika soko la muziki huo.
No comments:
Post a Comment