HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 07, 2014

BEN POL KUFANYA KAZI NA P SQUARE, J MARTINS


Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa taratibu ‘RnB’ nchini, Bernad Poul ‘Ben Pol’, amesema malengo yake katika tasnia hiyo ni kufanya kazi na wasanii wa kimataifa ili kukuza muziki huo kwa wadau na wapenzi wake.

Baadhi ya wasanii ambao Ben Pol amesema anatamani kufanya nao kazi ni kama, Peter na Paul Okoye ‘P.Square’, Martin Justice 'J.Martin', Kundi la Brackets, Timaya Ukwu 'Timaya' na wengine ambao wanafanya vizuri katika Bara la Afrika.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ben Pol alisema hiyo ni mipango yake ambayo anataka kuitimiza ndani ya mwaka huu baada ya kufanya vizuri mwaka uliopita.

Alisema mwaka jana ulikuwa ni mwaka wa mafanikio kwake, hivyo anataka kuendeleza mashambulizi kwa kufanya kazi na wasanii wa kimataifa na kuhakikisha anawashika mashabiki wengi tofauti na miaka iliyopita.

“Nina mipango ya kuboresha muziki wangu, kwa kufanya kazi na wanamuziki wa kimataifa napenda kuanza na wasanii wa Nigeria, kutokana na ukaribu ambao nipo nao kwasasa hivi, nikifanikiwa na hao itanibidi nizunguke katika nchi nyingine, hii yote ni kutaka kutimiza malengo yangu ya kuwa mwanamuziki mkubwa na kukubalika nchi zote za Duniani,” alisema Ben Pol.

No comments:

Post a Comment

Pages