Na Francis Dande
TAMASHA la Pasaka la mwaka huu litakalozinduliwa rasmi April 20, jijijini Dar es Salaam likibeba kaulimbiu ya ‘Tanzania Kwanza Haki Huinua Taifa,’ litaendeshwa chini ya staili ya wadau wenyewe kuchagua waimbaji iwe kutoka ndani au nje na mgeni rasmi.
Hayo yalibainishwa jijini
Dar es Salaam leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Msama Promotions waandaaji wa
tamasha, akisema wapenzi wa muziki huo ndio watawachagua waimbaji hao kwa
kutuma ujumbe mfupi kupitia namba 15327 kwa kutumia mitandao yote ya simu.
"Tamsha la mwaka huu linakuja kwa staili
mpya ambapo wapenzi wa muziki wa injili watakuwa na fursa ya kuwachagua
wanamuziki watakao penda waje kutoa burudani na mikoa litakapo fanyika tamasha
hilo tofauti na miaka mingine na wale wote watakao pendekezwa tutawaleta kutoa
burudani," alisema Msama.
Alisema, licha ya kuweka utaratibu huo, kumekuwa
na changamoto kubwa kutoka kwa wapenzi hao wa muziki wa injili ambao wanataka
wanamuziki waliotoa burudani wakati wa tamasha la Krismasi akiwemo Solly Mahalangu.
Msama alisema, maandalizi ya tamasha hilo
yamekamilika na katika mazingira ya kwenda na wakati, limekuwa na kaulimbiu ya ‘Tanzania
Kwanza Haki Huinua Taifa’.
Miongoni mwa waimbaji waliotikisa
Tamasha la Krismas ambalo lilizinduliwa rasmi Desemba 25, jijini Dar es Salaam
kabla ya kuhamia mikoani, ni Mahlangu, Ephraem Sekereti, Rose Muhando, Upendo
Kilahiro, Upendo Nkone na Edson Mwasabwite.
No comments:
Post a Comment