Na Kenneth Ngelesi, MBEYA
KOCHA msadizi wa timu ya Taifa ya
Tanzania Taifa Stars, Salum Mayanga (pichani), amezitaka timu zinazoshiriki Ligi Kuu
Tanzania Bara kutumia mji wa Tukuyu kama sehemu ya mazoezi ya maandalizi
kutoka na eneo hilo kuwa tulivu kwa ajili ya wachezaji.
Wito huo alitoa juzi Mjini Tukuyu
wakati wa mazoezi ya timu ya taifa ya Tanzania ambayo imepiga kambi mjini hapa
kwa ajili ya kujiwinda na mchezo wa marudiano dhidi ya timu ya Taifa ya
Msumbiji the Mambas unao tazamiwa kufanyika wiki ijayo.
Akizungumza na Tanzania daima
Kocha huyo alisema kuwa mazingira ya mji wa Tukuyu ni mazuri kwa
kupiga kambi iwe kwa timu ya taifa ama vilabu vya ligi kuu kwani hakuna bugza
kama ilivyo kwa Da-es-salaam.
Aliongeza ni vema kwa timu za
ligi mkuu kutimia maeneo kama yale kwani yanautulivu wa hali juu hivyo kumfanya
mchezaji kuwa makini wakati wote.
‘Unajua hawa wachezaji wetu wakiwa
jiji Dar-es-salaam wanakuwa na mambo mengi ikingatiwa wengine ni
wajaeriamalio hivyo kia mara wanaomba ruhusa kwenga kuangalia miradi yao
lakini kwa jhuyku ni ngumu hata linapo tokea tatizo anaishi kupiga simu, bali
angfkuwa Dar angelazimika kuomba ruhusa’alisema Mayanga.
Hata hivyo kocha huiyo alisema kuwa
anashangazwa na watu waloiko kuwa wanabeza uamuzi wa TFF kuatua mji huo kwa
jili ya kambi ya Stars kwani mazimngira yeki mazuri kuliko watu wanavyo dhani
kutokana na ulivu uliiopo.
Mbali na hali ya utulivu lakini pia
hali ya hewa katika mji wa Tukuyu nzuri hivyo ameviasa vilabu kutumia
mazingira kama hayo kwa ajili ya maandalizi kwa ajili ya michezo ya ligi
kuu hata vilabu vinavyo jiandaa na michezo ya kimataifa.
Akizungumzia hali ya kambi hiyo
Kocha huyo msadizi alisema kuwa ipo vizuri na ari ya wachezaji ipo juu na
kwamba jana timu hiyo ilitazamiwa kurejea jiji Dar es Salaam tayari kwa safari
ya kuelekea mjini Maputo kwa ajili ya mchezo wa marudiano.
No comments:
Post a Comment