Wajumbe wa mkutano wakimsiliza Mwenyekiti wa mjadala Dkt. Philip Mpango. Upande wa kulia ni wajumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na upande wa kushoto ni wajumbe kutoka serikali ya Japan. Picha na: Thomas Nyindo, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Wajumbe kutoka Serikali ya Tanzania wakifuatilia michango mbalimbali kutoka kwa wajumbe wa mkutano huo. Miradi iliyowasilishwa ilihusisha Sekta za Kilimo, Viwanda, Usafirishaji, Nishati, Maji, na Afya.
Baadhi ya wajumbe kutoka Tume ya Mipango, Klasta ya Biashara ya Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi ambao walioshiriki kuratibu majadiliano hayo kutoka kulia Bw. Robert Senya na Bi. Sudah Lulandala wakifuatilia mjadala wakati wa mkutano huo.
Wajumbe kutoka Serikali ya Japan wakichukua mambo ya muhimu wakati Mkutano wa Majadiliano ulipokuwa ukiendelea. Ujumbe huo uliongozwa na Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaki Okada.
Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip I. Mpango (wa pili kushoto) akifungua mkutano wa majadiliano baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Japan kuhusu ufadhili wa miradi ya maendeleo kwa mwaka 2014/15. Majadiliano hayo yalifanyika Julai 25, 2014 katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha na yaliratibiwa na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Wajumbe wa mkutano uliohusisha Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara, Wakurugenzi na Wataalam wa Sekta mbalimbali wakifuatilia kwa makini majadiliano yaliyokua yakiendelea.
No comments:
Post a Comment