Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB anayeshughulika na huduma
ya China Deski, Ibrahim Masahi (kulia), akitoa ufafanuzi kuhusu huduma maalum
za kibenki kwa ajili ya kusaidia wafanyabiashara na wawekezaji wa China na
Tanzania, wakati wa maonyesho ya bidhaa za China yaliyofanyika jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya wateja wakisoma vipeperushi vyenye taarifa muhimu za Benki ya CRDB kuhusu huduma maalum ya China Deski.
Baadhi ya watu waliofika katika banda la CRDB wakati wa maonyesho ya bidhaa za China wakisoma vipeperushi vyenye taarifa muhimu kuhusu huduma maalum ya China Deski.
Ibrahim Masahi akitoa ufafanuzi kwa wateja waliotaka kujua huduma za China Deski.
Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB anayeshughulika na huduma
ya China Deski, Ibrahim Masahi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma maalum
za kibenki kwa ajili ya kusaidia wafanyabiashara na wawekezaji wa China na
Tanzania, wakati wa maonyesho ya bidhaa za China yaliyofanyika jijini Dar es
Salaam.
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya CRDB, imeeleza kupata faida baada ya kuanzisha
deski la China kwa kuwaunganisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka China na
hapa nchini.
Akizungumza jana katika maonyesho ya bidhaa za China
Afrika, yanayofanyika jijini Dar es salaam, Meneja Uhusiano wa Deski hilo,
Ibrahim Masahi, alisema kuwa huduma hiyo imerahisisha na kuwasaidia
wafanyabiashara kupata mikopo na kufanya huduma za kibenki, kukuza wigo wa
kibiashara.
Masahi alisema kuwa huduma hiyo umuwezesha mteja wa CRDB
kutoa hadi kiasi cha sh milioni 40 kwa siku ikiwa atakuwa nchini China au
Tanzania kwaajili ya biashara na kuwekeza.
“Tangu kuanza kwa hudyma hii benki kupitia deski la China
imepata faida ya zaidi ya Bilioni 30, na imeunganisha wateja mbalimbali na
wawekezaji wanaonunua bidhaa china, lakini kwa upande wa Tanzania Chnagmoto
kubwa ni lugha wakiwa kule China na rate imekuwa ikibadilikabadilika,”alisema.
Aidha aliwataka watanzania kuchangamikia fursa hiyo ambayo
imeondoa madhara ambayo yangeweza kutokea na kueleza kuwa kwasasa wameingia
ubia na benki zaidi ya 10 nchini China.
No comments:
Post a Comment