HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 27, 2014

DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA SARATANI YA MATITI KUTOKA INDIA ATUA NCHINI

 Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira (kulia), akimtambulisha kwa madaktari (hawapo pichani), Daktari Bingwa wa magonjwa ya saratani ya matiti, Profesa Anthony Pais, kutoka Bangorole India,  Dar es Salaam jana. Daktari huyo kesho jioni anatarajia kufanya mhadhara na madaktari wa Kitanzania na wadau wa sekta ya afya kujadili ugonjwa huo katika Hoteli ya Protea Court Yard. Daktari huyo yupo nchini kwa mwaliko maalumu wa mshauri huyo wa Kimataifa.
 Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira (kulia), akiwa na daktari huyo (katikati), Kushototo ni Mama Benedicta Rugemalira.
 Profesa Anthony Pais (kulia), akizungumza na madaktari wa Tanzania.

Na Dotto Mwaibale

DAKTARI Bingwa wa ugonjwa wa saratani ya matiti , Profesa Anthony Pais, kutoka Bangorole nchini India kesho Agosti 28, 2014  anatarajia kutoa muhadhara kuhusu ugonjwa huo.

Akizungumza na Mtandao wa www.habari za jamii.com. Dar es Salaam leo Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira alisema ujio wa daktari huyo hapa nchini ni fursa kwa watanzania kutokana na changamoto kubwa iliyopo kuhusu ugonjwa huo.

"Daktari huyu amebobea katika ugonjwa wa saratani ya matiti na amefanya operesheni nyingi za ugonjwa huo ni wakati mzuri kwetu kwenda kumsikiliza kesho jioni Hoteli ya  Protea Court Yard" alisema Rugemalira.

Alisema kesho daktari huyo atatoa mhadhara kwa madaktari wa kitanzania na wadau wa sekta ya afya kuhusu ugonjwa huo na jinsi ya kukabiliana nao.

Rugemalira alisema daktari huyo atakuwepo nchini kwa siku kadhaa na leo alitembea Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Taasisi ya Kansa ya Ocean Road na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Daktari huyo yupo nchini kwa mwaliko maalumu wa mshauri huyo wa kimataifa ili kuona namna ya kusaidia tatizo hilo. 

No comments:

Post a Comment

Pages