HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 19, 2014

DK. EDMUND MNDOLWA: MSIWABUGHUDHI VIONGOZI WALIOPO MADARAKANI WAACHENI WACHAPE KAZI

Na Dotto Mwaibale

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wametakiwa kuacha kuwabugudhi viongozi waliopo madarakani kwa kuchaguliwa waendelee kuchapa kazi badala ya kuanza kuzihitaji nafasi zao kabla ya wakati.

Mito huo umetolewa na Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Chama hicho wilaya ya Korogwe mkoani Tanga Dk.Edmund Mndolwa wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo.

"Wito wangu kwa wanachama wenzangu wenye lengo la kutaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chama chetu wasianze kutamka nia ya kuwania nafasi hizo kabla ya wakati kwani kufanya hivyo ni kuwapunguzia kasi ya utendaji  viongozi waliopo madarakani.

Mndolwa alisema mtu anapotokea kuanza kuonesha nia kwa mfano wa kugombea ubunge katika eneo fulani kunamfanya mbunge aliopo katika eneo hilo kuacha kufanya shughuli za kuwatumikia wananchi badala yake anaanza kutumia muda mwingi wa kupambana na mtu huyo anayetaka kugombea kwenye jimbo husika.

Katika hatua nyingine Mndolwa amewataka watanzania kuendelea na mchakato wa Bunge la Katiba kwani ndio mahitaji yao badala ya kusitisha Bunge la Katiba linaloendelea mkoani Dodoma.

"Kwa mtazamu wangu ni vizuri mchakato wa bunge hilo ukaendelea kwani ndio mahitaji ya watanzania waliowengi kukomea njiani ni kupoteza mabilioni ya fedha za wananchi kutoka na vikao vinavyoendelea kufanyika" amesema Mndolwa.

Mndolwa amesema hivi sasa yupo katika ziara ya kutembelea mashina na matawi ya CCM wilayani humo kwa ajili ya kuimarisha uhai wa chama na kujua changamoto mbalimbali zilizopo ili kuziwasilisha ngazi ya juu kwa hatua ya utekelezaji.

No comments:

Post a Comment

Pages