Mwanamitindo
Flaviana Matata (wa tatu kutoka kulia waliosimama nyuma) akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya
Msingi Mnengulo mkoani Lindi. Jumla ya wanafunzi 650 wa shule zilizipo
katika Halmashauri za Lindi na Nachingwea mkoa wa Lindi wamenufaika na msaada huo wa
mabegi hayo yenye vifaa mbalimbali vya shule, msaada huo umetolewa kwa pamoja
kati ya PSPF na Taasisi ya Flaviana Matata. Kushoto ni Meneja Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa Mfuko
wa Pensheni wa PSPF, Costantina Martin.
Na Mwandishi
Wetu, Lindi
Mfuko wa
Pensheni wa PSPF kwa kushirikiana na Taasisi ya Flaviana Matata imetoa msaada
wa vifaa vya shule kwa wanafunzi walio katika mazingira magumu mkoani Lindi.
Flaviana
Matata ambaye ni mwanamitindo anayefanya nchini Marekani amekabidhi mabegi 650,
kila begi lina vifaa mbalimbali vya shule.
Vifaa vilikabidhiwa na Flaviana
Matata mwenyewe kwa baadhi ya wanafunzi
wa wilaya za Nachingwea na Lindi Mjini
Lengo la
msaada huo ambao umetolewa kwa pamoja kati ya Taasisi ya Flaviana Matata na
PSPF ni kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha kila mwanafunzi nchini
Tanzania anapata elimu akiwa na vifaa muhimu vinavyohitajika.
Hii ni mara ya pili kwa PSPF kwa kushirikiana na
Taasisi ya Flaviana Matata kutoa msaada huo kwa wanafunzi, mwaka jana
wanafunzi wa shule mbalimbali mkoani
Pwani walifaidika na msaada huo.
Mfuko wa
Pensheni wa PSPF umekuwa ukijihusisha katika kusaidia maeneo mbalimbali
yanayohitaji msaada ambao utaleta mabadiliko chanya kwa jamii ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment