NA
CLEZENCIA TRYPHONE
MSHAMBULIAJI mpya wa Simba, Raphaer Kiongera (pichani), amemwaga wino wino wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake mtaa wa
Msimbazi Kariakoo Jijini Dar es Salaam ili kutimiza idadi ya nyota watano wa
kigeni.
Kiongera mshambuliaji hatari wa timu ya KCB ya nchini
Kenya, ni miungoni mwa nyota wa kimataifa wapya waliokonga nyoyo za mashabiki
katika mchezo wao wa Jumamosi iliyopita dhidi ya Zesco ya Zambia.
Kiongera amemwaga wino leo tayari kwa kuvaa uzi wa Simba
ambapo yeye atakuwa akivalia jezi namba 12, ndani ya klabu hiyo na kuungana na
wenzake, Hamis Tambwe, Donald Musoti, Joseph Owino na Pierre Kwizera.
Anasema, yeye amekuja moja kwa moja kwa kuwa uongozi
umeridhishwa na yeye na ndo maana umempa mkataba wa miaka miwili, hivyo hatarajia kurejea kwao kwa sasa labda mpaka
atakapomaliza ligi, endapo watapewa mapumziko.
“Unajua mimi kazi yangu ni mpira, na tayari viongozi
tumemalizana na leo nimesaini
mkataba wa miaka miwili, kwa kuwa Simba wanahitaji huduma yangu ndani ya miaka
hiyo na mimi nitawafanya kazi kweli kweli,”anasema Kiongera.
Anasema, anamshukuru mungu kupata nafasi ya kusakata
kabumbu lake Tanzania, hasa katika timu kubwa kama Simba, kwani kulikuwa na
wachezaji wengi wa Kimataifa amewaona lakini yeye amepata nafasi, hivyo basi atahakikisha
anaitumia vema.
Anaongeza kuwa, licha ya kupoteza mchezo wa jumamosi, timu yao
ni nzuri na yeye atajitahidi ili kuhakikisha anakuwa na namba katika kikosi cha
kwanza ndani ya timu hiyo.
Wakati huo huo, mshambuliaji mwenzake wa Simba Hamis Tambwe
amewataka wanasimba kuwa na subira kwa kuwa huu ni mwanzo na ndio timu imeanza
kukutana pamoja kwa sasa, na wachezaji wapya ni wengi ambao wanahitaji kukaa
pamoja kwa muda huku akikubali kiwango cha Kiongera.
“Timu iko vizuri na kitendo cha kuja kwa Kiongera naimani
Simba itakuwa tishio msimu ujao, kwani namjua anajitambua na kujua nini
anakifanya awapo uwanjani, nimemuona na namjua,”anabainisha Tambwe.
No comments:
Post a Comment