Na Kenneth Ngelesi, MBARALI
MICHUANO ya soka ya Merere cup 2014 ilifikia tamati juzi huku
timu ya soka ya Kapunga FC kutoka kata Itambo ikiibuka bingwa na kuondoka na
kombe baada ya kuichapa timu ya Soka Motor Cycle FC kutoka kata ya Chimala kwa
jumla ya mabao 2-1 katika mchezo wa
fainali uliopigwa katika uwanja wa Chimala.
Mchezo huo ambao ulikuwa mkali huku wachezaji wa timu zote
mbili wakionyesha ufundi wa kusakata
soka, timu ya Kapunga ndiyo iliyo kuwa ya kwanza kuliona lango la wapinzani wao kupitia
kwa mchezaji Shavi Maketa ambaye dk 6 ya mchezo aliindikia timu yake bao la
kwanza.
Baada ya ya Kapunga FC kupata bao hilo liliamsha hasira kwa
wachezaji wa timu ya Waendesha bodaboda (Moter Cycle FC) kwa kujibu mashabulizi langoni mwa wapinzani dk
10 walipata bao la kufutia machozi lililowekwa kimyani na mchezaji Philipo Philipo kwa njia ya mkwaju wa
penanti iliyopatikana baada ya beki wa timu ya Kapunga kumungusha katika eneo
la hatari na hadi mapumziko mabao yalikuwa 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikisaka
goli la kuongoza hata hivyo Kapunga FC ndiyo walikuwa makini kuzitumia nafasi
kwani dk 75 ya mchezo waliandika bao la pili na la ushindi ambalo lilifungwa na
mchezaji Bahati Msofya na hadi dk 90 zinamalizika na mwamuzi Devid Malema
alipuliza filimbi ya mwisho Kapunga FC- 2 na Motor Cylce FC-1.
Katika fainali hizo timu ya Kapunga ilifanya mabadiliko kwa
kuwa toa Rajabu Alex,Meja Manyanya, Geofrey Philimon,na Frorence Chitoto huku
nafasi zao zikichukuliwa nma Mbaraka Muba,Maiko Michael,Exaurd Edward na Simon
Mwampamba.
Wakati huo huo timu ya Motor Cycle waliwatoa Minjiro Alimwene,Rajabu
Ngaile na Damas Elius huku nafasi zao zikichukuliwa na Joseph Ngondwa Baraka
Cheusi,na Mbaraka Muba.
Mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo ambao ulifanyika
katikia Uwanja wa Chimala Mgeni mgeni rasmi katika fasdinali hizo zilizo
andaliwa na shirika nla hifadhi za taifa (TANAPA) Kocha wa timu ya Mbeya City
Juma Mwambusi aliwa kabidhi washindi zawadi.
Zawadi hizo katika fainali hiyo bingwa alifanikiwa kuondoka
na Kombe,Fedha,shilingi lakini tano,seti mopja ya jezi,ma mpira mmoja Ungo wa
televisheni ulio tolewa na kampunio ya Azamu TV.
Mbali na zawadi hizo kwa mshindi wa kwanza lakini pia
waandaaji wa mashindano hao walitoa zawadi kwa mshindi wa pili ambao ni Motor
Cycle seti moja ya jezi,shilindi laki 300,000/ na mpira mmoja wakati msindi wa
tatu alizawadiwa shilingi laki mbili.
Akizunngumza mara baada ya kukabidhi zawadi Kocha Mwambusi
aliwapongeza waandaji wa michuano hiyo yenye lengo kumuenzi aliye kuwa Chifu wa
wakabila la Wasangu aliye itwa Merere pamoja kupiga vipa Ujangiri kwani
imesadia kuibua vipaji.
Mbali na hilo lakini pia aliwataka wachezaji kuendelea
kujituma katika michuano mbalimbali inayo andaliwa na wadau wa mchezo huo kwani
ndiyo njia pekee ya kuabaini vipaji vyao ambapo wakifanya vizuri itakuwa fursa
kwao kupata timu za ligi kuu.
Kwa upande wake mratibu wa michuano hiyo William Ndondole
alisema kuwa lengo la kufanyika kwa michuano hiyo ni kampeni za kupinga
ujangiri dhidi ya wanyamapori lakini kuwafanya vijana wasijiingize katika masuala
mouvu, na kwmba michuano hiyo iliyoshirikisha jumla ya timu 15 kutoka Wilaya ya
Mbarali ,ilidhamiwa na Benki ya Posta,Azam TV,TANAPA, kupitia Hifadhi ya Taifa ya
Ruhaha.
No comments:
Post a Comment