HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 01, 2014

Rotary Club yatoa msaada wa vifaa vya shule vyenye dhamani ya mili 14

Na KENNETH NGELESI, MBEYA

RAIS wa Shirika lisilo la kiserikali la "Rotary Club" ya Marekani tawi la Mbeya, Melas Mdemu, amesema njia pekee ya kumaliza changamoto zinazo ikabili Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi elimu ni jamii nyote pamoja na wadau katika wizara hiyo  kutambua umuhimu wa kuboresha miundombinu ya kujifunzia.

Mdemu alibanishwa wakati hafdla ya kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro  vitabu 1148 vyenye dhamani ya shilingi 7,551,000/ vya kujifunzia na kitabu kiongozi cha mwalimu katika shule ya Msingi Idida kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la kwanza hadi darasa la Saba.

Mbali za msaada huyo wa Vitabu lakini pia Klabu hiyo ilimkabidhi  madawati 120, meza tatu na vitu vitatu vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 7,200,000/ Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbasi Kandoro katika shule ya Msingi Songwe 2 zote za kutoka halmashauri ya Mbeya.

Alisema kuwa wadau wa elimu wanawajibu na kuhakikisha wanawasaidia wanafunzi wa shule ili watimize malengo yao ya kielimu na maisha kwa kuwajengea miundombinu rafiki ya kujifunzia kama vile madawati, vitabu na kujenga madarasa na vyoo bora.

Alisema endapo wadau wa elimu ambao ni serikali, wananchi na wahisani wakishirikiana kwa kushikamana katika kuboresha miundombinu ya elimu kuna uwezekano mkubwa kwa wanafunzi kufaulu vizuri katika masomo yao.

Akipokea msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Kandoro, alisema, msaada huo umesaidia kupunguza ongezeko kubwa la uhaba wa vitabu na madawati unaoukabili Mkoa wa Mbeya.

“Ndugu zangu erikali pekee haiwezi kutatua tatizo hili la uhaba wa vitabu vya kufundishia, kujisomea watoto pamoja na madwati, hivyo kitendo kilichofanywa na shirika hili, ni kikubwa na kinahitaji kuigwa na mashirika mengine,”alisema.

Aidha, Mkuu huyo aliutaka uongozi wa shule hiyo, kutumia vizuri msaada huo hasa katika kutimiza lengo halisi la kusaidia kupunguza wimbi la watoto wasiojua kusoma na kuandika.

Katika hatua nyingine Kandoro, alisema kuwa wazazi wengi waleonyesha mwitikio mkubwa katika ujenzi wa madasa na kwamba juhudi waliozo zieonyesha katika ujenzi huo ni vema pia wakageuzia katika ujenzi wa nyumba za walimu.

‘Ndugu wananchi napenda niwapongeza jinsi mlivyounga Mkono jududi za serikali wakati wa ujenzi wa madarasa hivyo basi juhudi hizo hizo ni vema pia mkazielikeza katika ujenzi wa nyumba za walimu’ alisema Kandoro.

Alisema kuwa madarsa pekee bila nyumba za walimu ambao kwa sehemu kubwa ndiyo wenye mchango mkubwa wa maendeleo mazuri ya mwanafunzi kitaalumu hivyo ni vema akawa na mazingira mazuri ya kuishi.

No comments:

Post a Comment

Pages