HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 01, 2014

Bilioni 8 kutumika ujenzi wa michezo wa kisasa Chunya

Na Kenneth Ngelesi, Mbeya
                                                
KAMPUNI ya Saruji Mkoani hapa “Mbeya Cement”  imetoa mifuko 1000 ya Saruji sawa na tani 50 kwa ajili ya kusaidia kuendeleza ujenzi wa Uwanja wa kisasa wa Michezo Wilayani Chunya.

Akizungumza katika hafla ya  makabidhiano iliyofanyika juzi mjini Chunya, mkurugenzi Mtendaji wa Mbeya Cement Catherin Langreney alisema  kuwa kiwanda hicho kimeamua kutoa mifuko hiyo ya saruji ikiwa utekelezaji wa ombi la mkuu wa wilaya hiyo Deudatus Kinawilo.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa baada ya Kampuni hiyo imetoa msaada wa mifuko ya saruji kutoka na ombi la Mkuu huyo ambaye  alionyesha kuwa na kiu ya kuwa na uwanja wa kisasa wa michezo katika Wilaya yake.

Akitoa shukrani mara baada ya kuopokea Msaada huyo Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa anaipongeza kampuni hiyo kwa kuwa moja ya wadau ambao wameshiriki kumaliza kiu ya muda mrefu ya  kuwa na uwanja wa michezo wa kisasa.

Mbali na kutoa shukrani hizo lakini pia  aliwataka wadau wengine kutoka wilaya hiyo na Mkoa kwa ujumla  kuunga mkono jitihada za wilaya hiyo kama ilivyo kwa kampuni ya Saruji ili kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa.

Akifafanua zaidi Kinawilo alisema kuwa mpaka sasa zaidi ya shilingi milioni 107 zimechangwa kutoka kwa wadau mbalimbali na kwamba  ujenzi wa uwanja huo unatarajiwa kukamikamika mwaka 2016.
Aidha katika hatua nyingine Mkuu huyo wa wilaya alibainisha kuwa jumla ya shilingi milioni 8 zinatarajiwa kutuma katika ujenzi wa uwanja huo.

Hata hivyo Tanzania daima imeshuhudia hatua za awali za kusafisha uwanja na ufyatuaji wa tofali zikiwa zimekamilika,za ujenzi wa uwanja huo ambao utakata kiu ya wananchi wa Chunya.

Chunya ni moja ya Wilaya Kongwe tangu utawala wa kikoroni na moja ya wilaya ye nye utajiri mkubwa wa madini kama dhahabu hapa nchini na  kinara wa kustawisha mazao mbalimbali ya chakula lakini suala la ukosefu wa uawanja wa michezo lilikuwa ni changamoto kwa maendeleo katika sekta ya michezo kwa ya wilaya hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages