Meneja Masoko wa Kampuni ya Mbegu ya (Seedco),
Frank Wenga akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini
Arusha juzi, kuhusu mashindano ya mashamba darasa katika Shule za Msingi
zilizopo Kanda ya Ziwa. Kushoto ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo, Daniel
Mwambugi. (Picha na Ferdinand Shayo)
Na Ferdinand Shayo, Arusha
Kampuni ya Uzalishaji mbegu ya SEEDCO imezindua mashindano
ya mashamba darasa kwa shule za msingi zilizopo katika mikoa ya kanda ya
ziwa ambapo shule itakayolima shamba
zuri itajishindia zawadi ya madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 15.
Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Frank Wenga amesema kuwa wameamua kufanya mashindano hayo baada ya kugundua changamoto
kubwa ya elimu katika somo la kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa uchumi wa nchi
hii ili kufikia malengo ya kufanya kilimo chenye tija ni vyema kuwafundisha Watanzania kilimo na wameamua kuanza na
wanafunzi wa shule za msingi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari amesema kuwa shindano
hilo ni mahususi kwa shule za msingi zilizopo mikoa ya kanda ya kaskazini ambayo ni
Kagera,Kigoma,Tabora,Geita, Shinyanga,Simiyu,Mwanza na Mara.
“Mbali na zawadi kuu ya madawati 100 yenye thamani ya
shilingi milioni 15 za kitanzania ,zawadi nyingine zitakuwa ni sare za
michezo,vibao vya kuandikia,madaftari na kalamu na pia mwalimu ambaye ataifanya
shule yake ishinde atazawadiwa simu ya kisasa ya mkononi” Alisema Meneja huyo.
Frank Wenga alisema kuwa fomu za kujiunga na shindano hilo
zitapatikana katika maduka ya mawakala yaliyothibitishwa kuuza mbegu za Seedco
na mwisho wa kujisajili ni August 30 mwaka huu.
“Kampeni hii ya mashindano imelenga kuwafundisha kilimo kwa
njia ya vitendo wanafunzi wa shule za msingi na kutoa zawadi zitakazowapa
motisha ya kupenda kilimo tangu wakiwa shuleni” Alisema Wenga
Anafafanua kuwa wanafunzi watajifunza kulima kwa kuzingatia
misingi ya kilimo bora cha kisasa ni
pamoja na kutumia mbegu bora,mbolea za kupandia na kukuzia na uhifadhi bora wa
mazao baada ya kuvuna.
No comments:
Post a Comment