SR1a: Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na M,ichezo Profesa Elisante Ole Gabriel akipokea zawadi ya maua kutoka kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi na Awali Sunrise ya jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya Saba ya wahitimu wa Darasa la Saba.
Mwanafunzi anayehitimu Darasa la Saba katika Shule ya Msingi na Awali Sunrise Bw. Mark Ngalo akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake wakati wa mahafali yao yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.Aliyemshikia kipaza sauti ni Lulu Benson.
SR1b. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi na Awali Sunrise ya jijini Dar es Salaam akito neno la kuwakaribisha wageni waliohudhuria mahafali ya wanafunzi wanaomaliza Darasa la Saba katika shule hiyo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na M,ichezo Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza na wazazi na wanafunzi wakati wa mahafali ya wahitimu wa Darasa la Saba wa Shule ya Msingi na Awali Sunrise ya jijini Dar es Salaam alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na M,ichezo Profesa Elisante Ole Gabriel akimkabidhi Cheti mmoja wa wahitimu wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi na Awali Sunrise ya jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya Saba ya Shule hiyo yalifanyka jana jijini Dar es Salaam. Katika ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Onesmo Vitalis.
Kikundi cha Skauti cha Shule ya Msingi na Awali Sunrise wakitoheshi mbele ya mgeni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (hayupo pichana) alipokuwa mgeni rasmi katika mahafa ya saba kwa wahitimu wa Darasa la Saba katika shule hiyo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Awali ya Sunrise wakifurahia kwa michezo wa sanamu wakati mahafali ya darasa la Saba jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wa Darasa la Saba wa Shule ya Msingi na Awali Sunrise ya jijini Dar es Salaam wakiwa wenye nyuso za furaha wakati wa mahafali yao.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na M,ichezo Profesa Elisante Ole Gabriel (waliokaa katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na wahitimu wa Darasa la Saba wa Shule ya Msingi na
Awali Sunrise ya jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi katika
mahafali ya Saba ya hiyo. Picha
zote na Frank Shija Afisa
Mawasiliano Serikalini, WHVUM.
Na Rose Masaka, MAELEZO
Watanzania waaswa
kuheshimu na jitihada za kukuza na kuendeleza Elimu zinazofanywa na wadau
mbalimbali hapa nchi zikiwemo sekta binafsi ambapo amesma sekta hii muhimu
ndiyo chimbuka la maadili mema kwa Taifa.
Rai hiyo imetolewa na Naibu
katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel
wakati akizungumza na wanafunzi na wageni mbalimbali katika mahafali ya Darasa
la Saba wa Shule ya Msingi na Awali Sunrise jana jijini Dar es Salaam.
Profesa Elisante
alisema kwamba Elimu ni suala mtambuka ambapo kila mwananchi mwenye mapenzi
mema na nchi yake ana wajibu wa kuenzi na kusaidia katika jitihada za
kuhakikisha sekta hii inakua bora zaidi ili kupata Taifa lenye tija.
Aidha Profesa Elisante
amesisitiza umuhimu wa wazazi kushirikiana kwa karibu na walimu ili kuhakikisha
wanafunzi wanapata Elimu iliyo bora ikiwema maadili mema.
“Ndugu zangu tunawenza
kabisa tukajenga Taifa lenye watu waadilifu kama tutashirikiana baaina ya
walimu na wazazi katika kuhakikisha watoto wetu wanapata Elimu iliyo bora,
hapana shaka kabisa msingi wa maadili mema huku ndiko unakoanzia” Alisema
Profesa Elisante.
Profesa Elisante
aliongeza kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa ,walezi,walimu na jamii kwa ujumla
kujenga utamaduni wa kuwafundisha watoto maadili mema, kwani hiyo itawasidia
kufikia malengo waliyokusudia.
Profesa Gabriel
aliongeza kuwa, ili kuwepo na elimu bora kuna mambo makuu ya kuzingatia kama uongozi wa shule mzuri
wenye mshikamano,wazazi au walezi kutimiza wajibu wao wa kazi na wanafunzi pia
kusoma kwa biidii ili kuwapa moyo wazazi wa kulipa ada kwa wakati
na walimu kufanya jitihada ya kufundisha.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Shule hiyo Bibi. Mary Shirima alisema kuwa Shule hiyo ilianzanisha
kwa lengo la kusaidia huduma za jammi ambapo Elimu ni moja kati ya huduma hizo.
Bibi. Shirima aliongeza
kuwa wao kama wananchi wa kawaidi wanatambua wajibu wa kusaidia jitihada katika kukuza maendeleo ya nchi ikiwa ni
kuonesha kwa vitendo dhana ya ushirikiana baina ya Serikali na Taasisi binafsi.
“Tulianzisha Sunrise
kwa utashi na dhana ya kutimiza wajibu wa kusaidia jamii kama mwananchi
anayeipenda nchi yake na wajibu wetu kama walezi, walimu na wafanyakazi wote wa
shule yetu kuhakikisha watoto wanaohitimu darasa la saba wanafikia malengo yao
ya baadae kwa kushirikiana na wazazi
wao”.Alisema Bibi Shirima.
Aidha Bibi. Shirima alisema kuwa imekuwa ni faraja
kwake kuona Serikali inatambua mchango wa wadau wanaojitolea kuwekeza katika
sekta mbalimbali ikiwemo elimu na kuelezea furaha yake kwa kiongozi wa ngazi ya
juu wa Serikali kukubali kuwa mgeni rasmi katika mahafali ya Darasa la Saba
ambapo Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo alikubali kuwa mgeni rasmi katika mahali hayo nakuwakilishwa
vyema na Naibu Kaitbu Mkuu wa Wizara hiyo.
Shule ya Msingi na
Awali Sunrise ilianzishwa mnamo mwaka 1999 ambapo hadi sasa inashereheke
mahafali ya Saba kwa wahitimu wa Darasa la Saba ambapo jumla ya wahitimu wa
mwka huu ni 66 kati yao Wasichana 42 na Wavulana
No comments:
Post a Comment