HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 02, 2014

CCM YASTUKIA USANII WA UKAWA


     Chama Cha Mapinduzi kimewastukia Ukawa na kusema wanachofanya ni Usanii usiokuwa na tija mbele ya mambo ya msingi kwa Taifa la Tanzania, akizungumza na mwaandishi wa habari hizi Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye alisema hoja zote zinazotolewa na UKAWA zina majibu kwenye Sheria na Kanuni zinazoendesha Bunge la Katiba ,CCM pia imewashukia  UKAWA kwa kuwatukana na kuwadhalilisha viongozi wa dini ambao wamekuwa wakisisitiza UKAWA kurudi Bungeni.


     CCM yawaomba wabunge wa bunge la Katiba wanaotaka Katiba mpya waendelee na bunge  litakapoitishwa tarehe 5/8/2014.


Kwa taarifa za ndani ya kikao hicho, kikao kimeisha kwa kutokubaliana, pande mbili hizi zimekutana zaidi ya mara nne pamoja na kikao cha leo kilichoanza asubuhi saa nne mpaka jioni lakini hakuna hata pande mmoja uliokubalina na mwenzake.


Kwa mujibu wa taarifa za ndani Msajili wa vyama vya Siasa  nchini anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari kesho jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages