HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 04, 2014

WAZIRI MKUU MSTAAFU FREDRICK SUMAYE AZINDUA ALBAM YA "SHIKILIA PINDO LA YESU" YA ROSE MUHANDO DIAMOND

1
Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akikata utepe wakati akizindua rasmi albam ya Rose Muhando mwimbaji wa muziki wa injili inyoitwa Shikilia Pindo la Yesu katika onesho kubwa la uzinduzi lililofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam leo likihudhuriwa na maelefu ya washabiki wa muziki wa injili, ambapo waimbaji mbalimbali wameshiriki katika uzindzi huo wakiwemo Ephraim Sekereti Kutoka Zambia, Sara K. kutoka Kenya , Upendo Kilahiro, Upendo Nkone John Lisu na wengine wengi, Katika uzinduzi huo pia maaskofu na wachungaji kutoka makanisa mbalimbali wamehudhuria, Katika anayeshirikiana na Mh. Ffredrick Sumaye ni Alex Msama Mkurugenzi wa ampuni ya Msana Promotion iliyoandaa uzinduzi huo na kushoto ni Mwimbaji Rose Muhando mwenyewe.
2 
 Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akionyesha Juu albam ya Shikilia Pindo la Yesu ya Rose Muhando mara baada ya kuizindua rasmi kulia ni Alex Msama Mkurugenzi wa Msama Promotion.
3
Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akimsikiliza Askofu Mwakibolwa wa makanisa ya Pentekosti akimkaribisha Mgeni rasmi Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredric Sumaye ili kuzungumza na waalikwa na washabiki mbalimbali wa muziki wa injili.
4
Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akisoma hotuba yake wakati alipozindua albam ya mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
001
Rose Muhando mwimbaji wa muziki wa injili akishirikiana na waimbaji wake wakati wa uzinduzi wa albam yae ya Shikilia Pindo la Yesu leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
01
Rose Muhando mwimbaji wa muziki wa injili akifanya vitu vyake wakati wa uzinduzi wa albam yake ya Shikilia Pindo la Yesu jijini Dar es salaam leo
6
Mashabiki mbalimbali wakiwa wamefurika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee
7
Mashabiki mbalimbali wakiwa wamefurika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee
8
Mwimbaji Upendo Kilahiro akiwa amekaa na Emmanuel Mbasha wakati wa uzinduzi wa Albam ya Rose Mundo ya Shikilia Pindo la Yesu.
9
Waimbaji wa mwimbaji Rose Muhando wakiwajibika jukwaani
11
Mwimbaji Sara K kutoka nchini Kenya aifanya vitu vyake jukwaani.
12
Upendo Nkone akikamua na Mumewe jukwaani ambaye alimtambulisha bila kumtaja jina kama wanavyoonekana.
13
Mwimbaji Jhn Lisu akifanya vitu vyake
14
Mwimbaji Upendo Kilahiro akiwa amekaa na Emmanuel Mbasha
15
Mgeni Rami Mh. Fredrick Sumaye wa pili kutoka kushoto pamoja na wageni wa meza kuu wakifurahia muziki wa injili utoka kwa mwimbaji Rose Muhando hayupo pichani.
16
Mwimbaji Ephraim Sekereti kutoka nchini Zambia akikamua mble ya wageni waalikwa
17
Mgeni Rami Mh. Fredrick Sumaye akimpongeza mwimbaji Rose Muhando mara baada ya kuzindua albam yake ya Shikilia Pindo la Yesu.
18
Mgeni Rami Mh. Fredrick Sumaye akiteta jambo na MC Mwakipesile aliyeongoza shughuli hiyo wakati wa onesho hilo la uzinduzi

No comments:

Post a Comment

Pages