Afisa Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile pamoja
na Meneja wa Kanda ya ziwa wa PPF Bwana Meshach Bandawe wakifuatilia mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika ukumbi wa Gold Crest kuwahabarisha kuhusu kampeni ya Mwanamke ya Uchumi itakayofanyika jijini Mwanza tarehe
4-5 Septemba, 2014 katika viwanja vya Mwaloni Kirumba Jijini Mwanza. (Na Mpiga Picha Wetu)
4-5 Septemba, 2014 katika viwanja vya Mwaloni Kirumba Jijini Mwanza. (Na Mpiga Picha Wetu)
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Angels Moment, Naima Malima akizungumza
na na waandishi wa habari kuhusu Kampeni ya Mwanamke na Akiba inayotarajiwa
kufanyika Mkoani Mwanza kuanzia Septemba 4-5, ambapo zaidi ya wanawake wajasiriamali
600 wanatarajiwa kufaidika na mafunzo hayo.

Afisa Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile akielezea
jukumu la TBS katika kuwaelimisha wanawake wajasiriamali wa Kitanzania watakaoshiriki katika kampeni ya Mwanamke na Uchumi juu ya ubora na viwango katika bidhaa wanazoandaa.
Afisa Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile
akielezea
jukumu la TBS katika kuwaelimisha wanawake wajasiriamali wa Kitanzania
watakaoshiriki katika kampeni ya Mwanamke na Uchumi juu ya ubora na
viwango katika bidhaa wanazoandaa.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Mwanza, Hamis Fakii
akielezea umuhimu wa akinamama kujiwekea akiba katika Mifuko ya Pensheni kwa Maisha yao ya sasa na ya baadae, Pia kujiunga na skimu ya SHIB ili wapate matibabu na familia zao kwa kuchangia pesa kidogo sana.
Afisa Huduma na Elimu wa TRA Mkoa wa Mwanza, utufyo Mtafya ambae ni akielezea umuhimu wa wanawake wajasiriamali wa kitanzania kutunza mahesabu yao kwa kutumia mashine za EFD.
Meneja wa Kanda ya Ziwa wa PPF, Meshach Bandawe
akielezea kwa wanahabari jinsi PPF inavyosaidia wanawake wajasiriamali walio katika sekta isiyo rasmi kwa kuwapa mikopo kupitia SACCOS.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Angels Moment, Naima Malima akizungumza
na na waandishi wa habari kuhusu Kampeni ya Mwanamke na Akiba inayotarajiwa
kufanyika Mkoani Mwanza kuanzia Septemba 4-5, ambapo zaidi ya wanawake wajasiriamali
600 wanatarajiwa kufaidika na mafunzo hayo.
Na Mwandishi Wetu
ZAIDI ya wanawake 600 mkoani Mwanza, wanatalajia kupata elimu juu ya ujasiriamali , Usimamizi wa fedha, uwekaji akiba pamoja na mafunzo ya afya bora.
ZAIDI ya wanawake 600 mkoani Mwanza, wanatalajia kupata elimu juu ya ujasiriamali , Usimamizi wa fedha, uwekaji akiba pamoja na mafunzo ya afya bora.
Akina
mama na vijana kutoka katika wilaya za
Magu, Ilemela, Misungwi na Nyamagana watashiliki kikamilifu katika kampeni hii itakayotolewa na
taasisi ya ANGELS MOMENTS ya jijini Dar es salaam.
Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Mwanza jana,Mkurugenzi
wa Taasisi ya ANGELS MOMENTS Naima Malima, alisema
kampeni hii inalenga kuwajengea uwezo na ujuzi wa kusimamia fedha zao
kwa lengo la kunyanyua uwezo wao wa kiuchumi pamoja na familia zao.
Naima
alisema kampeni hiyo imeanzia mkoani Mwanza kwa kutambua fursa zilizopo mkoani
hapo, hivyo wanawake wa mkoa huo watapewa elimu ya msingi ya kibiashara na
kuchochea na mna ya kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo ndani na
nje ya mkoa wa Mwanza.
“Kwa
kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii pamoja na taasisi ya WAMA
tunatarajia kuwafikia wanawake wa vikundi vyote vya kijamii, SACCOS, AMCOS,
VICOBA na makundi mengine ya kijamii yanayojihusisha na wajasiriamali na hivyo
kampeni hii itawawezesha kujiongezea uwezo wa kupata wateja wa bidhaa na huduma
zao na kujitangaza zaidi”. alisema Naima.
Aidha
alisema pamoja na mkoa wa Mwanza kampeni ya Mwanamke na Uchumi pia itafanyika
katika mikoa ya Tanga, Kigoma, Dodoma, Pwani, Ruvuma na Lindi kuanzia mwishoni
na mwanzoni mwa miezi ya septemba hadi Januari 2015 mtawalia.
Alimalizia
kwa kuwaomba wanawake na vijana wote wa mkowa wa Mwanza kufika bila kukosa
Septemba 4 na 5 katika viwanja vya Mwaloni, Kirumba jijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment