Na Ashura Jumapili, Bukoba,
MWANAFUNZI wa
kidato cha tano Ezra Gerald Wambamba (19 )wa kombi ya CBG katika
shule ya sekondari ya wavulana Ihungo
iliyoko Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera,
amejinyonga kwa kutumia shuka hadi kufa kwa madai ya kukosa huduma ya
matibabu akiwa hospitali.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kaimu Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Kagera, Gilles Muroto, amesema kuwa
tukio hilo lilitokea Septemba 16 mwaka huu majira ya saa moja, asubuhi katika hospitali ya Mkoa wa
Kagera, alikokuwa amelazwa mwanafunzi huyo anayetoka maeneo ya Kitete mkoani
Tabora.
Muroto,alisema, mwanafunzi huyo
alijinyonga kwaku tumia shuka hadi kufa
umbali wa mita 73 kutoka wodi namba tatu alikokuwa,amelazwa mwanafunzi huyo
alifunga shuka hiyo juu ya mti na
kujinyonga.
Alisema,alilazwa hospitali hapo
tangu Septemba 11 mwaka huu na
kugundulika kuwa anasumbuliwa na homa ya typhoid hadi 16 alipoamua kujinyonga.
Alisema,mwili wa marehemu, ulipopekuliwa
na jeshi la polisi alikutwa na kipandae
cha karatasi kilichoandikwa ujumbe unaosemeka hivi ”haiwezekani binadamu kuhudumiwa kama mbwa yaani nafika hospitali
najieleza hali yangu halafu daktari ananiandikia
kulazwa bila kupimwa,sasa sijui natibiwa nini?kwakweli
siwezi kuvumilia yaani wenzangu wanasoma halafu mimi nimekalishwa tu hapa hosipital bila ya kujua natibiwa nini?,inaniuma sana mpaka kufikia hatua hii kujiondoa duniani kwa sababu ninaona watu
wanachezea ndoto zangu
mimi siwezi kuona ndoto yangu inazimwa wakati
inatakiwa niwepo shuleni nikamilishe
ndoto zangu.”
Alisemabaada
yakuandikaujumbehuoakamaliziakwakusema “mjitahidi tukutane
mbinguni”mwishoakaandikanenolakiingereza( respect myfamily and Henry).
Aliongeza kuwa katika tukio hilo hakuna ,aliyekamatwa uchunguzi unaendelea kuhusiana na kifo hicho cha
mwanafunzi.
Kwa upande wake katibu wa hospitali
ya mkoa wa Kagera Benges Justus
alithibitisha kutokea kwa tukio la mwanafunzi
kujinyonga hadi kufa septemba 16 mwaka huu majira ya saa moja na nusu
asubuhi.
Benges,alisema mwanafunzi huyo alipokelewa hospitalini hapo septemba 15na baada
yakufanyiwa uchunguzi wa kitabibu wa vipimo vyote ilibainika kuwa anasumbuliwa
na maralia hivyo kuanzishiwa tibaya
maralia.
Alipohojiwa kamamgonjwa huyo alikuwa na typhoid alisema
vipimo vilionyesha maralia na siyo typhoid.
Hata hivyo alisema uchunguzi wa kifo
cha mwanafunzi huyo unaendelea ilikubaini kilichomuua. Chanzo cha habari Tanzania Daima.
No comments:
Post a Comment