HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 17, 2014

MWINYI KUFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA SEKTA YA UJENZI


Bwa. Jehad A. Jehad
Na Dotto Mwaibale

RAIS mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi kesho kutwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika  mkutano wa wataalam wa sekta ya ujenzi nchini ulioandaliwa na Bodi  ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB).

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam msajili wa AQRB, Jehad Jehad alisema mkutano huo ni muhimu kwa wataalamu hao katika kujua changamoto zilizopo katika sekta hiyo.

Alisema mkutano huo utafanyika kesho ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kuanzia saa mbili asubuhi.

"Mkutano huu ni muhimu sana kwete kutokana na changamoto nyingi zilizopo katika sekta ya ujenzi" alisema Jehad.

Alisema katika mkutano huo kutatolewa mada mbalimbali na wawezeshaji Mhandisi Dk. Ramadhan Mlinga kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mhandisi Julius Mamiro kutoka NCC na Nikodemus Komu kutoka Hexatech Consult.

Alisema mada zitakazo tolewa na wawezeshaji hao zimechaguliwa mahususi kuwapa fursa wadau katika sekta hiyo hasa wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kujadili changamoto wanazopata katika kutekeleza sheria ya Manunuzi namba 7 ya mwaka 2011.


"Mada hizi ni muhimu katika kuimarisha udhibiti wa matumizi ya fedha za umma katika sekta ya ujenzi" alisema Jehad.

Alisema pamoja na mada hizo kutakuwepo na maonesho mbalimbali kutoka kwa wadau wa sekta ya ujenzi hususani wafanyabiashara wa vifaa na huduma za ujenzi.

Jehad alitumia fursa hiyo kuwaomba Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi na wadau wengine wa sekta ya ujenzi kote nchini kushiriki katika semina hiyo muhimu ambao AQRB inawaomba waajiri wote nchini kufadhili ushiriki wa wataalamu wao wa sekta ya ujenzi kuhudhuria mkutano huo kwa manufaa ya taifa.

Alisema kauli mbiu ya mkutano huo ni Sheria ya Manunuzi namba 7 ya mwaka 2011 na athari zake katika Mazingira ya Ujenzi.

No comments:

Post a Comment

Pages