Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Umeme nchini (TANESCO), imesema tatizo la kukosekana kwa huduma
hiyo katika baadhi ya maeneo kulikojitokeza wiki iliyopita kulisababishwa
usafishaji wa visima vya gesi ya Songosongo.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi
Mkuu wa Tanesco, Flechesmi Mramba, alisema Kazi hiyo ilikuwa ikifanywa na
Kampuni Pan African ambayo ndio inayosimamia visima hivyo.
Alisema, kazi hiyo ilisababisha ratiba ya uaptikanaji wa gesi kubadilika
hali iliyofanya wakati mwingine wajikute hali yakukosa huduma hiyo.
Mramba, alisema kutokana na ratiba hiyo walilazimika kutumia mitambo ya
mafuta ili kuziba upungufu huo kutokana na mahitaji makubwa.
Hata hivyo kutokana na mahitaji hayo makubwa wakati mwingine Tanesco
imejikuta ikikosa mafuta hali iliyosababisha usumbufu kwa wateja.
"Tunawasilana na watu wa Songosongo wametuhakikishia kuwakazi ya
usafishaji visima hivyo inakwenda vizuri inaitamalizika, kufanaya tatizohilo
kumalizika kesho na kwamba tuwaombe radhi wateja na pia wajue sababu
iliyosabisha usumbufu huu,"alisema Mramba.
Aidha, alisema hivi sasa katika kumaliza matatizo ya umeme katika baadhi ya
maeneo Mbagala Tanesco imeamua kujenga laine nyingine kutoka Kipawa kwenda
Mbagala ambayo itasaidia laini inayotoka Ilala iliyozidiwa na wateja.
Baada ya kukamilika line hiyo anamini kuwa hali ya upatikanaji wa huduma
hiyo katika maeneo ya Mbagala na mengine itakuwa nzuri.
No comments:
Post a Comment