Mshambuliaji wa timu soka ya Mtibwa sugar Mussa Mgosi
akidhitiwa na Mabeki ya Mbeya City,Kenny Ally kushoto na Deogratius
Julius kulia katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa jana katika uwanja wa
Sokoine jiji Mbeya (Picha na Kenneth Ngelesi)
Beki wa timu ya Mbeya City, Deogaritus Julius akiambaa akimiliki mpira huku
akinyelewa na mshambuliajai wa Mtibwa Sugar, Mussa Mgosi katika mchezo
uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Kumbu kumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Wachezaji wa timu ya Soka ya
Mtib wa wakishanglia goli lao la kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu
ya Soka Tanzania Bara ulipigwa na katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Na Kenneth Ngelesi, MBEYA
TIMU ya Mtibwa Sugar, leo imeendeleza wimbi la
ushindi na kubaki kuwa timu pekee ambayo haijafungwa katika Ligi Kuu, baada ya kuifunga Mbeya City ya Hapa kwa mabao 2-0 katika pambano kali kwenye Uwanja wa
Sokoine.
Ushindi wa
leo umeiweka juu zaidi timu ya Mtibwa Sugar kwa toafuti ya pointi tatu, baada ya
kuifanya kufikisha pointi 13, huku ikiziacha Yanga na Azam FC zikibanana katika
nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 10 baada ya mechi tano tano kwa kila kikosi
tangu kuanza kwa msimu huu wa 2014/15.
Bao la kwanza
la Mtibwa Sugar lilifungwa dakika ya 20 na nyota wake Ame Ally, akiunganisha
kona iliyopigwa na beki wa kushoto wa zamani wa Yanga anayekipiga na ‘Wakata
Miwa’ hao kwa sasa, David Luhende. Baada ya bao, Mtibwa waliendelea
kuishambulia Mbeya City na nusura wapate bao la pili dakika ya 31 kupitia Ally
Shariff. hadi mapumziko, matokeo yalikuwa wageni kuongoza mechi
kwa bao hilo 1-0 dhidi ya wenyeji wao ambao msimu huu unaonekana kuwa mgumu
kwao.
Kipindi cha
pili kilianza kwa kasi ya aina yake Mbeya City wakipania kusawazisha bao,
ambako walianza na badiliko la kumtoa Themi Felix na nafasi yake kuchukuliwa na
Peter Malyanzi, ambaye nusura aipatie timu yake bao la kusawazisha, lakini
shuti lake dakika ya 53 lilidakwa na kipa wa Mtibwa Said Mohammed.
Dakika ya 76,
Mtibwa wakajihakikishia ushindi muhimu, kutokana na bao maridadi la Andrew
Vicent, alilofunga baada ya kuwalaamba chenga mabeki wa Mbeya City na kufumua
shuti kali na kumshinda kipa David Burhani.
Dakika moja
kabla ya filimbi ya mwisho ya mwamuzi Hashimu Abdallah wa Dar es Salaam, Mtibwa
nusura wapate bao la tatu, lakini shuti la adhabu ndogo nje ya boksi,
iliyotokana na Vicent kuchezewa rafu, kupaa nje ya lango. Hadi mwisho, Mtibwa Sugar 2 Mbeya City 0.
Vikosi katika
pambano hilo vilipangwa hivi, Mbeya City: David Burhani, Kenny Ally, Hassan
Mwasapili, Deogratius Julius, Yohana Morris, Yusuph Abdallah, Deus Kaseke,
Steven Mazanda, Paul Nonga, Saad Kipanga na Themi Felix.
Mtibwa Sugar:
Mtibwa Sugar, Said Mohammed, David Luhende, Salim Mbonde, Andrew Vicent,
Shabani Nditi, Mussa Hassan ‘Mgosi’, Mohammed Ibrahim, Ame Ally, Mussa Nampaka
na Ally Shariff.
No comments:
Post a Comment