HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 25, 2014

SITTI MTEMVU AJIVUA TAJI LA REDD'S MISS TANZANIA 2014

Kwa mujibu wa habari zilizowekwa katika mtandao wa kijamii wa Face Book Sitti Mtemvu ameamua kujivua Taji la Redd's Miss Tanzania  2014 kutokana na tuhuma  za kudanganya umri. Hata hivyo juhudi za kuwapata viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania kudhibitisha habari hizo zinandelea.
Haya ni maeneo yaliyoandikwa katika ukurasa wa Face Book ya Sitti Mtemvu

Habari za jioni watanzania wenzangu, kutokana na kuwa nimekuwa nikisemwa sana, maneno mengi yasio na tija juu ya hili taji la umiss tanzania 2014,,,mpaka kupelekea nisiwe na amani na uhuru ndani ya nchi yangu tanzania, kwa roho safi nimeamua mwenyewe kujivua taji hilo na kuacha wanaye ona anastahili taji hili apewe ili niendelee na maisha yangu kwa amani ,isiwe shida sana kwani sitegemei taji hili ili kuishi!!
Aliyekuwa Redd's Miss Tanzania2014, Sitti Mtemvu akiwa na mshindi wa pili na mshindi wa tatu mara baada ya kutangazwa kwa matokeo na majaji wa shindano hilo. 
 Aliyekuwa Redd's Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu akipokea zawadi yake ya mfano wa hundi ya sh. milioni 10.
Redd's Miss Tanzania 2014 akipongezwa na baba yake, Abass Mtemvu (MB)

1 comment:

Pages