HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 23, 2014

BMTL yaja na mashine za kutuma fedha benki

Meneja Mkuu wa BMTL, Deepak Kumar Khara akizungumza wakati wa hafla ya utambulisho wa bidhaa mpya za kampuni hiyo.
 Baadhi ya wageni waalikwa.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya BMTL, Mike Holtham akizungumza wakati hafla ya utambulisho wa bidhaa zao mpya za mashine za kisasa za kuhesabu fedha na makasha maalum ya kuhifadhia fedha.
 Mashine za kisasa za kuhesabia fedha.
Mashine za kisasa za kuhesabu fedha.
 Baadhi ya mashine za kisasa za kuhesabia hela.
 Makasha maalum ya kuhifadhia fedha.
Wasanii wakitumbuiza katika hafla hiyo.
Leyla akimtangaza mshindi wa bahati nasibu.
 Mshindi aliyejishindia zawadi za bidhaa zenye thamani ya sh. 500,000, Sravan Kumar (kulia)  akipokea zawadi yake kutoka kwa Mkuu wa Mauzo, Avais Ansari. 
Agatha Bugomola akipokea zawadi yake kutoka kwa Mkuu wa Mauzo, Avais Ansari. 


Mhandisi wa Kampuni ya Business Machines Tanzania Ltd (BMTL), Salum Nyambe akitoa maelezo  kuhusiana na mashine za kisasa za kuhesabu fedha pamoja na teknolojia mpya ya kudhibiti wahalifu ikiwemo kutuma fedha bila kwenda benki. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.

Mhandisi wa Kampuni ya Business Machines Tanzania Ltd (BMTL), Salum Nyambe (kulia) akionyesha mashine za kisasa za kuhesabu fedha wakatikampuni hiyo ilipotambulisha teknolojia mpya ya kudhibiti wahalifu ikiwemo kutuma fedha bila kwenda benki. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.

Mashine za kisasa za kuhgesabia sarafu.
 Mhasibu Mkuu wa Kampuni ya BMTL, Zakarioa Kijula akizungumza na waandishi habari wakati wa hafla ya
Makasha ya kuhifadhia fedha.
Meneja Maendeleo Biashara Mashariki ya Kati wa Kampuni ya Glory Global Solution, Joop Schouten (kulia) akiwa na Mhandisi Kamau Thuo. 
Mkuu wa Mauzo, Avais Ansari wa BMTL akitoa maelezo kuhusu mashine hizo kwa wageni waliofika katika hafla hiyo.

Mkuu wa Mauzo, Avais Ansari wa BMTL akitoa maelezo kuhusu mashine hizo kwa wageni waliofika katika hafla hiyo. 

Na Mwandishi Wetu

WAKATI wahalifu wakiwa wanabuni mbinu mpya kila kukicha za kuiba katika benki, kampuni Business Machines Tanzania Limited (BMTL), imekuja na mashine mpya za kuwadhibiti wahalifu ikiwemo ya kutuma fedha bila kwenda benki.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam, katika hafla ya kuonesha mashine hizo mpya za kutuma, kuhesabu na kuhifadhia fedha, Meneja Uhasibu wa kampuni hiyo, Zakaria Kijula, alisema wamekuja na teknolojia hiyo mpya ili kusadia kuwaweka wateja wao salama.

Kijula alisema kama kampuni wanajua wazi kwamba huwezi kuendesha akili ya mtu lakini unaweza kuidhibiti hivyo kwa wezi wa benki wameona ni vema kubuni mashine mbalimbali zitakazowezesha wateja wao kufanya kazi katika mazingira yaliyo salama.

Akielezea kuhusu mashine ya kutuma fedha bila ya mteja kulazimika kwenda benki, alisema itamsaidia kupunguza usumbufu na gharama kubwa ya kuweka walinzi wakati wa kuzisafirisha fedha hizo.

Badala yake alisema kupitia mashine hiyo mteja ataweza kudumbukiza kiasi chochote cha fedha atakachotaka kuweka benki akiwa ofisini kwake na kuingia moja kwa moja kwenye akaunti yake.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha mauzo wa kampuni hiyo, Avais Ansari, alisema katika kuendelea kuwaridhisha wateja wao watakuwa wakija na teknolijia mpya kila uchwao lengo likiwa si tu kupata fedha bali kuwaweka salama.

Mbali na mashine za kuhufadhia na kuhesabia fedha, alisema wamekuwa wakisambaza mashine za kutambua noti bandia na za kuhesabia sarafu.

No comments:

Post a Comment

Pages