Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hab Mkwizu
(katikati), Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Crescentius Magori (kulia) na Meneja Idara za Serikali na Balozi NSSF,
Rehema Chuma wakiwasili kwenye ukumbi wa mikutano wakati wa semina ya wadau wa
Kada ya Utumishi wa Idara na Asasi za Serikali iliyoandaliwa na NSSF mjini
Bagamoyo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori
akitoa akifafanua jambo wakati wa semina ya wadau wa Kada ya Utumishi wa Idara na
Asasi za Serikali iliyoandaliwa na NSSF na kufanyika mjini Bagamoyo, mwishoni
mwa wiki. Wa pili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma, Hab Mkwizu, Meneja
wa Idara za Serikali na Balozi NSSF, Rehema Chuma na
Meneja wa NSSF Mkoa wa Kibaha, Ummy Lweno.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hab Mkwizu akitoa
hotuba yake wakati wa ufunguzi wa semina ya wadau wa Kada ya Utumishi wa Idara
na Asasi za Serikali iliyoandaliwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF) na kufanyika mjini Bagamoyo.
Meneja
wa Idara za Serikali na Balozi NSSF, Rehema Chuma akizungumza katika semina hiyo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya
Jamii (NSSF), Crescentius Magori akitoa
mada wakati wa semina ya wadau
wa Kada ya Utumishi wa Idara na Asasi za Serikali iliyoandaliwa na NSSF na
kufanyika mjini Bagamoyo.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
Washiriki wa semina wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwakilishwa.
Wadau wa NSSF wakiwa katika mkutano huo.
Maofisa wa NSSF wakiwa katika mkutano huo.
Maofisa wa NSSF wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa.
Meneja
wa Idara za Serikali na Balozi NSSF, Rehema Chuma (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Chiku Matesa.
Mgeni Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hab Mkwizu (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma, Hab Mkwizu akiagana na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori mara baada ya kufungua
semina ya wadau wa Kada ya Utumishi wa Idara na Asasi za Serikali iliyoandaliwa
na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kufanyika mjini Bagamoyo
jana. Katikati ni Meneja Idara za Serikali na Balozi NSSF, Rehema Chuma.
Na Mwandishi Wetu
NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma, Hab Mkwizu, amewataka waajiri na wanachama wa Shirika la Hifadhi ya Jamii
(NSSF) kujadili changamoto zinazokabili shirika hilo na kuzitatua.
Mkwizu aliyasema hayo mjini Bagamoyo katika
semina iliyoandaliwa na NSSF ikiwa ni utaratibu wa shirika hilo kukutana na
wadau wake.
Alisema kuwa dhana nzima ya hifadhi ya jamii bado haieleweki
kwa wafanyakazi wengi na hiyo ni moja ya changamoto inayokabili mifuko hiyo
ndani ya nchi.
Mkwizu alisema changamoto nyingine ni wanachama kustaafu
bila kujua ni mfuko upi wanapaswa kwenda kufungua madai yao pensheni.
Aliwataka NSSF kutumia semina hiyo kutoa elimu na uelewa juu
ya dhana nzima ya hifadhi ya jamii, shughuli za shirika na mafao yanayotolewa kwa
wanachama, tararibu za kujiunga na taratibu za kufungua madai baada ya
mfanyakazi kustaafu.
Meneja wa Idara za Serikali na balozi NSSF, Rehema Chuma,
alisema semina hiyo ni uendelezaji wa elimu kwa wananchi na waajiri, kujenga
mahusiano ili kushughulikia maslahi ya wafanyakazi, kuelewa na kujadili
changamoto mbalimbali za sekta hii.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori,
alisema changamoto zitakazopatikana
zitasuluhishwa na kuongeza kuwa NSSF ni mfuko unaotoa mafao ambayo mifuko
mingine haina likiwemo fao la uzazi na matibabu.
No comments:
Post a Comment