Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Emmanuel Humba akisalimiana na wafanyakazi wa mfuko wakati wa hafla ya kumuaga ambapo Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (Tughe) tawi la Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF), kimemkabidhi zawadi ya sh. milioni 10 aliyekuwa Mkurugenzi
Mtendaji wa mfuko huo, Emmanuel Humba kutokana na kuthamini mchango wake kabla
hajastaafu.
Mwenyekiti wa Chama
cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (Tughe) tawi la NHIF, Gabriel Ishole (kushoto)
akimkabidhi tuzo maalumu Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya (NHIF), Emmanuel Humba kutokana na kuthamini mchango wake kabla
hajastaafu. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Emmanuel Humba akimkabidhi mke wake tuzo maalumu aliyopewa na wafanyakazi wa NHIF baada ya kustaafu.
Champagne zikifunguliawa.
Furaha ilitawala ukumbini.
Cheers kwa afya.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Khamis Mdee akigonganisha glasi na Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa mfuko huo, Emmanuel Humba.
Wafanyakazi wakigonganisha glasi kwa furaha.
Kila mtu alikuwa na furaha.
Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa mfuko huo, Emmanuel Humba (kushoto) akigonganisha glasi na wafanyakazi wa mfuko huo.

Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa mfuko huo, Emmanuel Humba (kulia) akigonganisha glasi na wafanyakazi wa NHIF.
Ofisa Elimu kwa Umma wa NHIF, Grace Michael (kushoto) akigonganisha glasi na Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa mfuko huo, Emmanuel Humba.
Wafanyakazi wakifurahi kuagana na Mkurugenzi wao.
Wafanyakazi wa NHIF wakicheza kwaito
Kwaito ilipamba moto.
Kila mtu alionyesha kipaji cjake.
Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa mfuko huo, Emmanuel Humba akisakata rhumba.
Wadau wa NHIF wakitafakari
Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa mfuko huo, Emmanuel Humba akipata chakula cha jioni.
Mke wa Mkurugenzi Mtendaji mstaafu akipata chakula.
Katibu wa Tughe tawi la NHIF, Gaudensi Kandyango akipata
Maofisa wa NHIF wakipata chakula cha jioni.
Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Emmanuel Humba akitoa neno la shukrani wakati wa hafla hiyo.
Wafanyakazi wakimtakia mkono wa pongeza Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Emmanuel Humba kwa kazi nzuri aliyofanya kabla hajastaafu.
Wafanyakazi wa NHIF wakicheza muziki.
Mwenyekiti wa Chama
cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (Tughe) tawi la NHIF, Gabriel Ishole (kushoto) akimkabidhi risiti ya ya Benki ya thamani ya shs. milioni 10 zilizotokana na michango ya wafanyakazi kwa upendo wao kwa Mkurugenzi wao mstaafu, Emmanuel Humba.
Wafanyakazi wa NHIF wakimpa cheti maalumu kwa kutambua mchango wake.
Kamati ya maandalizi ikiwa katika picha ya pamoja.
Kaimu Mkurugenzi Mktendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Khamis Mdee (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha kumbukumbu Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa NHIF, Emmanuel Humba.
Kaimu Mkurugenzi Mktendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Khamis Mdee (kushoto) akimkabidhi picha ya kumbukumbu Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Emmanuel Humba.
Pokea picha ya kumbukumbu.
Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa NHIF akipokea zawadi.
Picha ya pamoja.
Wafanyakazi wa NHIF wakiwa na zawadi kwa ajili ya kukabidhi mke wa Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa NHIF.
Pokea zawadi mama.
Mke wa Mkurugenzi mstaafu wa NHIF akishukuru kwa zawadi alizopewa na wafanyakazi wa Mfuko huo kutokana na kuthamini mchango wa Mkurugenzi wa NHIF, Emmanuel Humba.
Wafanyakazi wa NHIF wakiwa na furaha.
Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa mfuko huo, Emmanuel Humba na mke wake wakifurahia jambo.
Mwenyekiti wa Tughe tawi la NHIF, Gabriel Ishole akizungumza katika hafla hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NHIF akitoa neno.
Maofisa wa NHIF.
Meza Kuu.
Wafanyakazi wa NHIF.
Wadau wa NHIF.
Wafanyakazi wa NHIF.
Mwenyekiti wa Chama
cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (Tughe) tawi la NHIF, Gabriel Ishole akisoma risala.
Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Emmanuel Humba akionyesha tuzo aliyokabidhiwa.
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha
Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (Tughe) tawi la Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF), kimemkabidhi zawadi ya sh. milioni 10 aliyekuwa Mkurugenzi
Mtendaji wa mfuko huo, Emmanuel Humba kutokana na kuthamini mchango wake kabla
hajastaafu.
Humba ambaye pia
alikuwa muasisi wa chama cha wafanyakazi katika mfuko huo, alikabidhiwa risiti
ya fedha hizo juzi jioni jijini Dar es Salaam katika hafla ya kumuaga
iliyoandaliwa na wanachama wa Tughe, tawi la NHIF ambao pia ni wafanyakazi wa
mfuko huo.
Akizungumza kabla
ya kumkabidhi risiti hiyo, Mwenyekiti wa Tughe, tawi la NHIF, Gabriel Ishole,
alisema fedha hizo ambazo tayari yameshamuingia katika akaunti yake benki ni
kwa ajili ya kununulia mifuko 300 ya saruji, vigae na tiles, ili aweze
kuboresha makazi yake.
Kabla ya
kumkabidhi risiti hiyo, Ishole alimkabidhi zawadi ya tuzo, ili kuonyesha namna
wanavyothamini mchango wake katika mfuko huo kwa kuinua maslahi ya watu wa
chini.
Humba
aliwashukuru wanachama hao na kusema wameonyesha hekima kubwa na kwamba si kitu
cha kawaida walichomfanyia kwa kuwa mtu anapokuwa kiongozi huwa anakwaruzana na
wafanyakazi wengi.
"Mmenipa fundisho
muhimu sana, wafanyakazi mpaka wakualike! Najua wengi tulikwaruzana na nawajua,
lakini tulikuwa tunagombana kwa misingi ya kazi. Nawashukuru sana," alisema.
Mbali na hilo,
aliwaasa wafanyakazi hao kufanya kazi kwa kuheshimiana, ili mfuko huo uweze
kupanuka zaidi na kuwahuduma Watanzania wengi.
Alisema watumishi
hao wana deni mbele ya wanachama na familia zao na kwamba njia sahihi ya
kulilipa ni kufanya kazi kwa bidii kwa kutoa huduma stahiki kwa washika dau
wao.
“Wanachama, watoa
huduma ni wadau muhimu sana tuwaheshimu
tunaowahudumia na kwa misingi hiyo mtajipatia heshima…fanyeni wajibu wenu na
watu wawashukuru kwa hilo kuliko kubeba
viroba vya pesa,” alisema.
No comments:
Post a Comment