HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 26, 2014

USIKU WA KHANGA PARTY NOV 29

Na Andrew Chale
ASIA Idarous Khamsin na Safari Carnival wanakuletea usiku wa Khanga Party na Spice Modern Taarab watakaowasha moto wa burudani sambamba na gwiji wa mipasho nchini Khadija Kopa pamoja na Bilal Mashauzi, Jumamosi ya usiku wa Novemba 29, ndan ya ukumbi wa Safari Carnival, Mikocheni B.
Kwa mujibu wa mmoja wa wandaaji wa usiku huo, Asia Idarous Khamsin, amesema tayari maandalizi yake yamekamilika na amewasihi wadau kujitokeza kwa wingi katika onesho hilo la aina yake kwa kiingilio cha sh 10,000 na 20,000 kwa V.I.P. 

 Asia Idarous Khamsin alisema Usiku wa Khanga, itaanza kuanzia usiku wa saa mbili na kuendelea huku vazi maalum likiwa ni Khanga.
"Usiku huu ni maalum kulienzi vazi la khanga, ambalo pia ndilo vazi maalum la usiku huo. Pia watafurahia muziki mzuri kutoka kwa magwiji wa taarab hapa nchini akiwemo Khadija Kopa, Spice Modern taaba na Bilal Mashauzi." alisema Asia Idarous Khamisin ambapo pia alisisitiza vazi la khanga ni la heshima hasa kwa mwanamke wa Kitanzania hivyo kila mmoja atakapolitengeneza vizuri ama kufunga litamweka malidadi. 

 Aidha, alibainisha kuwa, usiku huo pia kutakuwa na zulia jekundu 'Red Carpet' ambapo watu mbalimbali watapata kupiga picha na mastaa na watu maalufu watakao jitokeza usiku huo. 

 Pia alibainisha kuwa, tayari tiketi zimeanza kuuzwa sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam ikiwemo Fabak fashions Mikocheni na Safari Carnival.
 kwa mawasiliano piga 0754263363 au 0713263363

No comments:

Post a Comment

Pages