HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 19, 2014

WATATU WAKAMATWA NA DOLA FEKI ZA MAREKANI ZENYE THAMANI YA SH. MILIONI 20

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Fresser Kashai akiwaonyesha waandishi wa habari mkoani hapa Dola Feki za kimarekani. Picha na Elizabeth Kilindi, Tanga.
Dola feki za Marekani.

 
Na Elizabeth Kilindi, TANGA
 
WATU watatu wanaojishughulisha na biashara ya uuzaji wa noti bandia mkoani Tanga wamekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa wakiwa na dola za kimarekani zenye thamani ya 11200 ambazo ni sawa na shilingi milioni 20 za Kitanzania .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Fresser Kashai aliwaambia waandishi wahabari leo kuwa watuhumiwa hao walikamatwa Novemba 17 mwaka huu saa saba na nusu eneo la barabara ya kumi na sita Kata ya Ngamiani wilayani Tanga  wakati kwenye harakati za kuziingiza kwenye mzunguko.

Alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa na Polisi wakiwa kwenye gari lenye Chasis namba JLg 100037726 ambazo ni wakazi wa Jijini Dar es Salaam wakiwa na noti hizo bandia ambazo walikuwa wamezificha

Aliwataja watuhumiwa wanaoshikiliwa na Jeshi hilo kuwa ni Julius
Kanza (30), kabila Mchaga na Mkazi wa Ubungo,Kenedy Binagi(35) mkazi wa Sinza na wa tatu ni Ramadhani  Saddy(33) kabila Muha na mkazi wa Mwenge

Kamanda Kashai alisema kuwa baada ya watuhumiwa hao kukamatwa walikiri kuhusika na biashara hiyo ambapo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili mara baada ya upelekezi wa awali kukamilika.

Wakati huo huo,Jeshi la Polisi Mkoani Tanga linaendesha msako mkali wa kuwatafuta wahusika wa matukio ya mauaji ya Mkulima mmoja yaliyotokeaKijiji cha Nyadigwa Kata na Tarafa ya Kimbe wilayani Kilindi.

Kamanda Kashai alisema kuwa tukio hilo la mauaji hayo lilitokea Novemba 18 mwaka huu majira ya saa kumi na moja na dakika arobaini na tano katika eneo la kijiji cha Vyadigwa Kata ya Kimbe wilayani humo.

Akizungumzia tukio hilo,Kamanda Kashai alisema mkulima wa Vyadigwa alikutwa porini akiwa amejeruhiwa maeneo ya utosini kwa kitu chenye ncha kali na watu wasiojulikana hali iliyomsababishia kifo chake.

Alisema kuwa mkulima huyo alifariki dunia saa kumi jioni wakati akiwakwenye hospitali Teule ya wilaya ya Kilindi (KKT) ambapo chanzo cha mauaji hayo bado kinachunguzwa .

No comments:

Post a Comment

Pages