HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 13, 2014

BW. GEORGE SHINGA MTAMBALIKE KUUFANYA MTAA WA MOGO KIPAWA KUWA WA KISASA

1
 Mgombea wa Uenyekiti wa Mtaa wa Mogo kupitia Chama cha Mapinduzi Bw. George Shinga Mtambalikeakizungumza na waandishi wa habari huko Ukonga majumba siti wakati akizungumzia juu ya kameni za uchaguzi huo ambazo zinatarajiwa kufungwa kesho kabla ya uchaguzi kufanyika jumapili Desemba 14.
2
Mgombea wa Uenyekiti wa Mtaa wa Mogo kupitia Chama cha Mapinduzi Bw. George Shinga Mtambalikeakizungumza  na vijana mbalimbali wakati alipokutana nao katika ukumbi wa Kiota Ukonga jijini Dar es salaam.
………………………………………………………………………
IMEBAINISHWA kuwa endapo wananchi wa kata ya Kipawa Mtaa wa mogo watakichagua Chama cha Mapinduzi CCM kupitia 

Mgombea wake George Shinga Mtambalike,basi mtaa huo anampango wa kuufanya kuwa mtaa wa kisasa kama ilivyokuwa mitaa mingine Duniani.

Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam jana na Mgombea wa Chama cha hicho kwa nafasi ya uwenyekiti wa Serikali ya Mtaa 

wa Mogo,wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini.

Alisema kuwa wananchi kama watampa nafasi ya kuwa kiongozi wao katika mtaa huo wa mogho basi malengo yake ni kuona 

Mtaa wa Mogo unakuwa katika sura ya tofauti ambapo pia atahakikisha mtaa huo unapimwa na kuwa katika mipango miji.

“Kimsingi wananchi wa Mtaa huu wanatakiwa wasifanye makosa wahakikishe wanakichagua chama cha Mapinduzi ili kuweza 

kutimiza ndoto za maendeleo katika mtaa huu wa Mogo ambao kwa muda mrefu umekuwa ukikabiliwa  na changamoto za 

kutosha,’alisema Mtambalike

Alisema kuwa mbali na kubadilisha mtaa huo pia atahakikisha kuwa makundi yote yaliyopo katika mtaa huo yanakuwa 

katika utambuzi ili kuweza kuzifikia kwa uhalaka fursa zinazojitokeza kupitia Ofisi ya Serikali ya Mtaa.

Akizungumzia miundombinu alisema kuwa kumekuwepo na changamoto kubwa ya miundombinu hivyo hatua ya kwaza baada ya 

kuingia madarakani ni kuhakikisha mazingira yanakuwa safi kwa maana ataunda vikundi mbalimbali ya kuzoa taka pamoja 

na kuimarisha ulinzi shiriki na utekekelezaji huo wote utafanywa na wakazi wa mtaa husika wa mogo.

Alisema kuwa malengo yake mengine ni kuona mtaa huo unamiliki Studio kwa ajili ya vijana,wanajenga Soko la kisasa 

ambalo kwa sasa wananchi wanapata shida na wanalazimika kwenda Buguruni kwa ajili ya kufata mahitaji yao muhimu ya 

nyumbani.

“Katika kuhakikisha haya yote tunakwenda kuyafanya basi ni muhimu wakazi kukichagua Chama cha Mapinduzi Disemba 14 

siku ya Juma pili ambapo vituo vitafunguliwa kuazia saa 2 asubuhi,’alisisitiza.

No comments:

Post a Comment

Pages