HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 01, 2014

MAABALA ZAWALIZA WAFANYABIASHARA

BAADHI ya Wafanyabiashara wa Kata ya Mabibo wilayani Kinondoni, Dar es Salaam wamelalamikia kiwango kikubwa cha fedha wanachotakiwa kuchangia katika ujenzi wa maabara za Shule za Serikali za kata.

Uchangiaji wa ujenzi wa maabara hizo unatokana na agizo la Rais Jakaya Kikwete ambapo zilitakiwa hadi Novemba 15 ziwe zimekamilika, hata hivyo bado ujenzi huo unakabiliwa na changamoto mbalimbali kutoka kwa wananchi.

Hayo yalisemwa jijini, Fatuma Khamis kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake wakati walipozungumza na wandishi wa habari kuhusu uamuzi huo kandamizi, uliofikiwa na uongozi wa kata hiyo.

Alisema kiwango wanachotakiwa kuchangia  ni vikubwa ambacho anaamini kutokana na biashara zao hawata weza kuvilipa hali itakayosabisha mgogoro wa kufikishana mahakamani kitendo ambacho kitakuwa sawa na kuwaonea.

“Huu uchangiaji, kila mfanyabiashara katika eneo letu hili utalingana na biashara zetu tunazofanya, pia tunalalmikia hivi viwango kwa sababu vimeamulia bila ya kushirikishwa”alisema

Alivitaja viwango wanavyo paswa kuchangia kulingana biashara husika, kama vile baa na nyumba ya kulala wageni sh 50,000, baa sh 25,000, Grosary sh 10,000 na nyumba ya kulala wageni sh 25,000.

Nyingine ni bekary ya mikate sh 50,000, duka la rejareja sh 5,000, Saloon ya kike na kiume sh 5,000 na biashara nyinginezo ambazo hazikufafanuliwa sh 10,000.

Mtendji wa Mtaa wa Kanuni, Juma Shaban ambaye alisema utekelezaji wa kazi hiyo hiyo ni agizo kutoka kwa wakubwa wao.

“Hili zoezi kweli linachngamoto lakini kikubwa kinachotumika ni busara katika ukusanyaji michango hiyo kwa sababu sisi huku miataani tunajuana hali za vipato vyetu,”alisema Shaban.

Alisema kweli wakati mwingine kuna kuwa na misuguano lakini hiyo inatokea mara chache, kwani kuna baadhi yao huwa wanatoa lugha chafu kwa mfano mtu anasema hatatoa fedha kwa sababu kazi ya serikali ni kula fedha zao tu.

“Hizo ni changamoto wanazokumbana nazo hata hivyo, inapotokea hivyo tunajaribu kutafuta njia ya kupata muafaka kwa sababu mtu anaposhindwa kulipa kiwango hicho hata akitoa nusu yake tunapokea lakini hadi sasa hakuna alifikishwa mahakamani,”alisema Shaban

Kuruthum Msimika ambaye ni Mtendaji wa Mtaa wa Mabibo Farasi, alisema katika mtaa wake hajapokea malalamiko kama hayo, huku akibainisha kwamba wanaendelea kulipa.

No comments:

Post a Comment

Pages