Mbunge wa
Chalinze, Mheshimiwa Ridhiwan Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye
uzinduzi wa mazoezi ya Bendi ya Wakulima inayoundwa na wanamuziki wakongwe
nchini.
Mbunge huyo
ambaye ni mmoja wa wadau wakubwa wa muziki hapa nchini, atazindua mazoezi hayo
yanayofayika kwenye ukumbi wa Jengo la Serikali ya Mtaa wa Kilwa, Ilala jijini
Dar es Salaam ambako bendi hiyo imepiga kambi.
“Kwa heshima
na taadhima Bendi ya Wakulima inakuomba uzindue rasmi mazoezi yake”, inasema
sehemu ya barua ya bendi hiyo iliyosainiwa na Katibu wake, Gregory Ndanu.
Ndanu
anazidi kusema kuwa uzinduzi wa mazoezi
hayo natazamiwa kuwa Desemba 14 mwaka huu.
Zaidi ya
hayo, Ndanu anasema katika barua hiyo ya maombi kwa Ridhiwan kuwa bendi hiyo
imetoa heshima hiyo kubwa kwake ikijua fika kuwa ni mdau mkubwa wa wakulima na
wafugaji kutokana na jimbo analoliongoza kuwa na wakazi wengi wa kada hiyo.
Bendi ya
Wakulima inaundwa na wanamuziki saba chini ya uongozi wa mkongwe wa kupapasa
kinanda nchini, Abdul Ali Salvador.
Salvador
ambaye awali alikuwa akijulikana kwa jina la uanamuziki la “Father Kidevu” kwa
sasa anajuikana kama “Dakta Savador” kutokana na ufundi mkubwa katika kusakata
kinanda na fani nzima ya muziki.
Wengine kwenye
bendi hiyo ni mwanadada supa, Nanah Mwashiuya maarufu Vampire (muimbaji),
Mfundo Juma “Mzumio” (muimbaji), Juma Membe (Mpiga solo),
King Mafanya (Mpiga
besi), Alphonce Paulo ambaye anapiga Drums na ,wama,uziki machachari na mwenye
mvuto mkubwa, Christian Sheggy.
Kwa mujibu
wa Ndanu,Bendi ya Wakulima ni mkombozi mkubwa kwa wakulima na wafugaji nchini
kwa vile imeanzishwa ili kutoa elimu kuhusu umhimu wa kilimo na ufugaji wa
kisasa kwa njia ya nyimbo na mapambio.
Aidha, bendi
hiyo itakuwa ikiishajiisha serikali na vyombo vingine kuthamini kilimo na
wakulima nchini kwa kuwa ndio haswa mhimili mkubwa wa uchumi na maendeleo binafsi
na ya jumla hapa nchini.
No comments:
Post a Comment