SIRI ya mgogoro wa kutaka kuwafukuzwa
wakazi wa vijiji vya Chanika wilayani Ilala jijini Dar es Salaa kwa madai kuwa
wamevamia msitu wa Kazimzumbwi yabainika.
Hayo yaliyasemwa na Mjumbe wa Kamati ya
wakazi na wakulima wa vijiji hivyo, Hamza Khamisi, alipozungumza kuhusu propaganda hizo zinazosambazwa na Wizara ya Maliasili na
Utalii, tangu mwaka 1992.
Alisema, siri ya kufukuzwa wakazi hao inatokana
serikali kuingia makubaliano na kampuni moja ya kigeni (jina tunalo), kutoka
nchini Norway hivi karibuni kwa ajili ya kuanzisha mradi ambao haujawekwa wazi.
“Kihistoria na kisayansi eneo la
Chanika na vijiji vyake vya Nzasa, Kimwani na Nyeburu sisehemu hata kidogo ya
msitu wa hifadhi ya Kazimzumbwi,”alisema Khamisi.
Alisema ikumbukwe kuwa baada ya
makubaliano hayo ndipo wizara ya Maliasili na Utalii ilipoamua kimabavu kuanzisha
mgogoro huo, bila ya kufuata utaratibu wa kisheria, kupanua mipaka yake kinyume
na ule wa asili wa mwaka 1954.
“Kamati yetu ywa wakulima imekuwa
ikishawishiwa kwa fedha ili ikubali kuwashauri kuwashauri wenzetu tukubali
kuondoka kwamba tutalipwa vizuri jambo linalotupa wasiwasi.
“Ndugu mwandishi tunayo CD ya mkutano
kati yetu na viongozi wa ngazi ya juu, uliyofanyika Kibaha, viongozi wakidai kupoteza
mradi huo wa wazungu nchi itapoteza fedha nyingi jambo ambalo itakuwa aibu kwa
nchi.
“Ninachoeleza wala sio madai tumefanya
vikao viwili vinavyowahusu hao wazungu cha kwanza ilikuwa Buguruni na hcho cha
mkoani pwani viongozi waliokuwepo watakapoona hii taarifa hawataweza
kubisha,”alidai Khamisi.
Aliyekuwa
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza, likakaririwa na vyombo vya habari
akisema serikali ya mkoa wake imeshapokea maelekezo ya serikali na itatekeleza
agizo hilo ambalo litasaidia kuirejesha misitu hiyo katika hali yake ya
kawaida.
Alisema
uharibifu huo umelitia aibu taifa mbele ya jumuiya ya kimataifa ambayo
inatambua umuhimu wa misitu ya Kazimzumbwi kimazingira na kuboresha hali ya
hewa ya jiji la Dar es Salaam.
Mwanzoni
mwa Desemba mwaka huu jijini katika
mkutano wa kitaifa wa msitu huo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Razalo
Nyalandu, alisema kamwe serikali haiwezi kuendelea kuwavumilia wavamizi hao
ambao wamesababisha uharibifu mkubwa wa mazingira ya misitu hiyo ya Kazimzumbwi
iliyohifadhiwa kisheria tangu mwaka 1954 na
Nyalandu
aliongeza kuwa katika operesheni hiyo kubwa itakayofanyika baadae mwezi huu
serikaili haitatambua hati au vibali vya watu wanaoishi katika misitu hiyo
kwani wanaishi humo kinyume cha sheria na ametaka watu wote humo kuanza
kuondoka kwa hiari kabla ya muda huo na amebadilisha hati zote zinazotumiwa na
wavamizi hao.
No comments:
Post a Comment